.................
Timothy Marko
Mamlaka ya Biashara nchini(Tantrade) imewatahadharisha wafanyabiashara wanaofanya Maonesho ya Bidhaa zao nje ya nchi pasipokuwa na idhiniya Mamlaka hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari na wahariri wa vyombo vya Habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Mamlaka ya kibiashara ya Tanzania (Tan trade) Latifa Khamis amesema kwa mujibu wa sheria 4 ya taasisi hiyo inazuia Taasisi kufanya maonesho yakibiashara ya bidhaa nje yanchi pasipo kuwa na kibali cha Mamlaka hiyo.
"Kuna watu wanafanyaMisafara ya kibiashara bila kibali Maaluum".Alisema Mkurugenzi wa tan trade Latifa Mohamed.
Latifa Mohamed alisema Lengo la sheria hiyo nikudhibiti na kukuza taswira yanchi na sekta ya Bidhaa na kibiashara nje ya nchi.
Alisema katika kipindi cha mwaka 2022/23 taasisi hiyo imekusanya milioni 40 ikiwa nalengo lakusanya milooni52 kwa mwaka 2023.
"Hadi sasa tumeweza kufanya utafiti wa masoko kwaMazao yakibishara katika nchi za Saudiarabia, kenya , Comoro,Malawi pamoja na Afrika yakusini"Aliongeza Latifa Mohamed.

Post a Comment