*******
Timothy Marko.
KATIKA kuhakikisha Masuala ya Ulinzi na usalama baina ya Tanzania na Msumbiji yanaimarika Waziri wa Ulinzi na jeshi la kujenga Taifa Dk Stergomana Tax pamoja na Waziri wa Mambo ya ndani wa Msumbiji Pascoal Pedro Joao Ronda wameingia Makubaliano juu ya Masuala ya Ulinzi na usalama baina ya nchi hizo.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga Taifa Dk Stergomena Tax amesema lengo lamashirikiano hayo katika masuala yaulinzi na usalama baina nchizo mbili nikuhakikisha Tanzania na Msumbiji wanatokomeza kabisa matukio ya kigaidi kwenye nchi zao.
"Ulinzi na usalama baina ya Tanzania na Msumbiji imekuwa nikipaumbele katika Mashirikiano yetu hasa katika kukabiliana na Vitendo na Matukio ya kigaidi ilikuwezesha Shughuli za kiuchumi zinafanyika katika hali ya kiusalama".Alisema Waziri wa Ulinzi na jeshi lakujenga Taifa Dk.Stergomena Tax.
Dk.Stergomena alisema nchi ya Msumbiji na Tanzania wamekuwa na Mahusiano ya Mda mrefu tangu harakati za kupigania uhuru hivyo mahusiano ya nchi hizo yamekuwa yakiimarika siku hadi Siku.
Alisema Makubaliano ya ulinzi na usalama baina ya Tanzania na
Msumbiji yamekuwa yakilenga sio tu ulinzi na usalama balihata kuwa wezesha Wananchi wanchi hizo kuweza kufanya shughuli za kiuchumi.
"Ugaidi umekuwa ni tishishio kwa Baadhi ya Nchi za kiafrika ,Mashirikiano haya yanalenga kukuza usalama naulinzi baina ya Nchi zetu hizi mbili Msumbiji na Tanzania ilikuwawezesha Wananchi wetu kufanya Shughuli za kiuchumi ilikujiletea Maendeleo"Aliongeza Dk Stergomena Tax.
Naye Waziri wa Mambo ya Ndani wa Nchi ya Msumbiji Pascol Pedro Ronda amesema kuwa Ushirikiano wa Masuala ya ulinzi na usalama kutawezesha sekta za usafirishaji na shughuli za kijamii kuimarika kati ya Msumbiji naTanzania.
Alisema Uhusiano wa Kidiplomasia kati ya Msumbiji na Tanzania niwa kipindi kirefu kupitia makubaliano hayo kutawezesha nchi hizo kupanga mikakati ya kiusalama ya Mda Mrefu.
"Ilikuwa na Maendeleo ya kiuchumi tunahitaji kudumisha masuala ya ulinzi na usalama kwenye Nchi zetu"Alisema Waziri wa Mambo yandani wa Msumbiji Pascoal Pedro Joao Ronda.



Post a Comment