TANZANIA YATOA POLE KWA LIBYA NA MOROCCO.


.............................

Timothy Marko.

Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki January Makamba ametoa pole kwa Wananchi wa Libya na Morocco kwa majanga waliyoyapata hivi karibuni nakusisitiza Kuwa Tanzania itaendelea kukuza ushirikiano wake na Nchi za Umoja wa Afrika nazile zilizopo kusini Mwa Afrika.

Akizungumza katika Mkutano wa Mabalozi wanaoziwakilisha Nchi zao hapa nchini jijini Dar es salaam  waziri wa Mambo ya Nje na ushikiano wa Afrika Mashariki January Makamba amesema kuwa   lengo la Tanzania nikukuza Mahusiano ya kidiplomasia katika nyanja za kiuchumi kwa Mabalozi wanaoziwakilisha Nchi zao hapa nchini.

" Lengo la kutanisha Mabalozi katika Mkutano huu nikujenga Mahusiano ya kidiplomasia kwa Mabalozi wanao ziwakilisha nchizao hapa nchini ,Nazile taasisi za kikanda hapanchini".Alisema Waziri wa Mambo ya Nje January Makamba.

Waziri Makamba alisema kuwa hivi karibuni Serikali kupitia wizara ya Mambo ya nje imepanga kufanya mabadiliko ya Sera ya Mambo ya nje ambayo awali sera hiyo ilianza kutumika 2001.

Alisema kuwa Mabadiliko ya sera ya Mambo ya nje ambayo itakamilika mwaka huu italenga kukuza masuala ya Dispora katikakukuza uchumi.

"Mambo Mengine yatakayo zingatiwa katika sera hii ya mambo ya Nje nipamoja na Ujirani Mwema,Utalii".Aliongeza Waziri Makamba.

0/Post a Comment/Comments