....................
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro Judith Nguli ameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Kwa kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu kutoka katika Wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya Ngulo ametoa Kauli hiyo wakati akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa vikundi vya kujitolea vya wananchi wa kukabiliana wanyamapori wakali na waharibifu ambayo imefanyika katika kijiji cha Mlela ambapo pia Hafla hiyo ilihudhuriwa na watumishi wa TAWA (Kanda Maalum ya Dar es Salaam) wakiongozwa na Kamanda wa Uhifadhi SACC Sylivester Mushy ambaye aliandamana na baadhi ya wahifadhi kutoka Kanda hiyo.
Katika Hafla hiyo pia uliofanyika ugawaji wa vifaa vya kufukuza tembo filimbi.(115); vuvuzela(115) ; vilipuzi mbalimbali vilivyotolewa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kwenye kata nne za Mlali,Melera, Mlali na lubungo katika wilaya ya Mvomero.
DC Nguli katika hotuba yake amewapongeza TAWA kwa utendaji mzuri wa kazi ya kuthibiti wanyamapori wakali na waharibifu
“ Nampongeza sana Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mushy, muda wote ukimpigia simu hata SÃ a 8 usiku anapokea na kupokea maagizo yangu, na yuko Dar es Salaam lakini muda huo anawatuma askari wake na kufika eneo la tukio na yeye kesho yake anafuatilia,Nampongeza sana Kamishna na wasaidizi wake”Nanukuu.
Naye Kamanda wa Uhifadhi SACC Sylivester Mushy amesema kuwa TAWA imejenga vituo 16 vya kuthibiti wanyamapori hapa nchini na pia inaendelea kutoa elimu Kwa wananchi kupitia mikutano ya wananchi na vyombo mbalimbali vya habari




Post a Comment