*******
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imekabidhi katoni 3878 za Pombe aina ya Chief kwa Jeshi la Magereza ili iweze kuwachangamsha Askari baada ya Kazi.
Akikabidhi vinywaji hivyo kwa Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Magereza Tanzania Lazaro William wa niaba ya Kamishina wa Jeshi hilo Mzee Ramadhani,
Afisa Mwandamizi wa Forodha kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania Victoria Tarimo, .amesema viamesema pombe hizo ni sehemu ya mzigo ambao upo kwenye mamlaka hiyo ambapo waliweza kushauri kwa Serikali na kupelekwa kwenye Jeshi hilo
Amesema wao Kama Taasisi ya Serikali yenye jukumu la kukusanya Mapato, imeona vyema kukabidhi mzigo huo ambao wahusika walikwama kuulipia Kodi.
Akizungumza mara baada ya kupokea mzigo huo Kamishina Msaidizi wa Magereza Lazaro William ameshukuru kwa msaada huo na kuomba kwa Mamlaka hiyo inapotokea fulsa nyingine kama hiyo au zaidi ya hiyo kuweza kuliangalia tena Jeshi hilo la Askari Magereza.




Post a Comment