Kamishina wa Forodha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Juma Hassan akizungumza na waandishi wa Habari juu ya uboreshaji wa Mazingira ya Biashara Bandarini mapema jijini Dar es salam leo.
Baadhi ya Mawakala wa forodha na washiriki wa mkutano wa forodha jijini Dar es salaam.
.....................
Timothy Marko.
KATIKA kuhakikisha Mazingira yaufanyajiBiashara yana imarika,Mamlaka yaMapato nchini (TRA) imekutana na jumuhia ya wanachama Ushuru wa Forodha nchini (TAFA) kuweza kujadili changamoto za utoaji wa mizigo Bandarini ilikuhakikisha mazingira ya Biashara yanaimarika nchini.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada yakikao hicho jijini Dar es salaam Kamishina wa forodha wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) Juma Hassan amesema kikao hicho kina lenga kuthimini mazingira ya Biashara na utendaji kazi wa Mawakala wa forodha nchini ilikuweza kutenda kazi kwa ufanisi.
"Lengo la Mkutano huu nikusisitiza utunzajiwa taarifa juu ya mawakala wa forodha pindi wanapotekeleza majukumu yao ilikuzuia makosa katika utendaji wao"Alisema Kamishina wa Forodha Juma Hassan.
Kamisha wa Forodha Juma Hassan alisema kuwa kikao hicho kina lenga kurahisisha Huduma za kiforodha hapanchini ilikuwezesha Uchumi wa nchi kukua .
Naye Muwakilishi wa Mawakala wa Forodha nchini TAFA Emanuel Kazimoto amesema Mkutano huo umekuja wakati muafaka kwani utaweza kunufaisha shughuli za kiforodha na huduma za sekta hiyo katika ukuwaji wa Uchumi nchini.
"Mkutano huu unalenga kukuzamahusiano kati ya Mawakala wa Forordha katika kuchangia ukuwaji wa uchumi nchini"Alisema Wakala Forodha Emanuel Kazimoto.



Post a Comment