Timothy Marko
ASASI ya Vijana wa Umoja wa Mataifa Tanzania(YUNA) kwa kushirikiana na Makumbusho ya Taifa Tanzania imeandaa kongamano la kitaifa Vijana juu ya urithi wa kitamaduni linalotarajiwa kufanyika Jumba la Makumbusho ya taifaSeptembar 27 Mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Mjumbe wa Kamati tendaji wa UNA Maadhisho hayo Irene Kijangwa amesema kuwa katika kongamano hilo lenye kaulimbiu "Asili yangu Fahari yangu" lina lenga kuwa Elimisha juu ya uhifadhi urithi nchini, juu ya utamaduni na utalii endelevu.
"Mkutano huu unalenga kuwa wezesha Viongozi Vijana kuwa wasimamizi wa urithi wetu nawashirikisha vijana kuwawasimamizi wa urithi wetu nawashirikihai katika kukuza utalii Endelevu na kuhifadhi hazina kitamaduni".Alisema Mjumbe wa kamatitendaji Irene kijanbgwa.
Irene kijangwa alisema kuwa dhima ya mkutano huo nikuongeza uelewa wa vijana juu ya hatuazinazoweza kuchukuliwa katika uhifadhi urithi wa kiutamaduni.
Alisema lengo la kongamano hilo linalenga kukuza uelewa wa vijana juu ya uhifadhi wa utamaduni na utalii endelevu.
"Kongamano hili linalenga kuwapa vijana juu ya uelewa juu ya hatua zinazochukuliwa katika uhifadhi wa urithi wa kitamaduni na kuwahamasisha vijana hao juu ya uhifadhi wa kitamaduni"Aliongeza Irene kijangwa.


Post a Comment