YARA KUZINDUA LISHE YA MIFUGO





*****

Kampuni ya uzalishaji wa bidhaa za kilimo ya YARA Tanzania leo inatarajia kuzindua bidhaa ya lishe ili kuboresha mifugo  kwa kuinenepesha zaidi na kuleta tija kwa wafugaji.

Lishe hiyo itatumika katika aina saba ikiwamo ng'ombe, mbuzi, jamii ya ndege pamoja na Samaki.

Hayo yameelezwa na leo Jumanne Septemba 19,2023 na Meneja wa Masoko Yara Tanzania na Rwanda, Sarah Munema alipokuwa akizungumza na waandishi wa habafi mkoani Iringa.

Kwa mujibu wa Munena, uzinduzi wa lishe hizo unatarajiwa kufanyika mkoani hapa katika ukumbi wa Gentle Hill.

Kwa  upande wake Mkuu wa Mkoa wa Iringa , Halima Dendego amepongeza uzinduzi huo ambao utakuwa chachu katika Utunzaji wa mazingira. 

Kabla ya uzinduzi huo, ujumbe wa YARA umefanya ziara katika Kiwanda cha Maziwa cha Asas na kuzungumza na Mkurugenzi Mtendaji Salim Faraj Abri.

Pia walitembelea kiwanda cha Mayai cha mfugaji mzawa cha Kefa Sanga kilichopo Igombelo na baadaye kutembelea kiwanda cha kuzalisha Mbegu za Mahindi cha Seedco cha Farm for The Future kinachomilikiwa kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania na Norway.

0/Post a Comment/Comments