AJENDA YA UTAFITI NCHINI INAKWENDA KUWA KUBWA SANA - DKT. JAFO

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa NORAD wa Programu ya Utafiti kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi sambamba na utiaji wa saini wa makubaliano ya usaidizi kati ya COSTECH na NORAD ambayo imefanyika katika ukumbi wa Tume hiyo leo jijini Dar es salaam.Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt Amos Nungu akizungumza na Balozi wa Norway nchini Tanzania Tonne Tines katika uzinduzi wa mradi wa NORAD wa Programu ya Utafiti kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi  sambamba na utiaji wa saini wa makubaliano ya usaidizi kati ya COSTECH na NORAD ambayo imefanyika katika ukumbi wa Tume hiyo leo jijini Dar es salaam.Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt Amos Nungu akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa NORAD wa Programu ya Utafiti kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi sambamba na utiaji wa saini wa makubaliano ya usaidizi kati ya COSTECH na NORAD ambayo imefanyika katika ukumbi wa Tume hiyo leo jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nungu na Mkurugenzi Msaidizi katika Kitengo cha Utafiti Elimu ya Juu Bi. Solbjorg Sjoveian wakisaini makubaliano ya ushirikiano katika ufafiti wakati wa hafla ya uzinduzi wa Programu ya Utafiti kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi kupitia Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) leo jijini Salaam. 
Baadhi ya wadau ambao wameshiriki uzinduzi wa mradi wa NORAD wa Programu ya Utafiti kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi na utiaji wa saini wa makubaliano ya usaidizi kati ya COSTECH na NORAD ambayo imefanyika katika ukumbi wa Tume hiyo leo jijini Dar es salaam
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali pamoja na wadau wa masuala ya utafiti wakati wa hafla ya uzinduzi wa Programu ya Utafiti kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi kupitia Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) leo Oktoba 11, 2023 jijini Dar es Salaam.
......,...............
 NA MUSSA KHALID

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo ameipongeza Tume ya Sayansi na Teknolojia nchini (COSTECH) kwa kufanikisha usimamizi wa kufanya tafiti zinazolenga kupambana na mabadiliko ya Tabianchi.

Waziri Jafo ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam wakati akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa NORAD kuhusu Programu ya Utafiti Kwa ajili ya Mabadiliko ya Tabianchi  sambamba na utiaji wa saini wa makubaliano ya usaidizi kati ya COSTECH na NORAD ambayo imefanyika katika ukumbi wa Tume hiyo.

Dkt Jafo pia ametumia fursa hiyo kuipongeza serikali ya NORWAY na SWEDEN kwa kushirikiana vyema na serikali ya Tanzania katika upande wa mabadiliko ya Tabianchi hasa kwenye utafiti.

Aidha Dkt Jafo amesema Tanzania imepata fedha zaidi ya Bill. 9 kutoka serikali ya NORWAY na SWEDEN kwa ajili ya shughuli za kufanya utafiti nchini kwani ajenda ya tafiti nchini inakwenda kuwa kubwa.

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt Amos Nungu amesema kuwa Matokeo yanayotarajiwa ya programu hiyo ni kutumia maarifa husika ya msingi wa utafiti juu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kupunguza mabadiliko ya jamii katika ngazi mbalimbali za Tanzania.

"COSTECH inaahidi kutumia vyema fedha hizo ili kukidhi mahitaji malengo ya programu, matokeo na matokeo kama ilivyoainishwa katika Ruzuku Hati ya Makubaliano, ambayo itatiwa saini siku hii. Tutafanya daima kutambua, kutathmini na kupunguza hatari zozote zinazohusika na utekelezaji wa programu na kuzipunguza ipasavyo"amesema Dkt Nungu

Ametumia fursa hiyo kusema kuwa Fedha zitatumika kikamilifu kufikia malengo ya programu, matokeo na matokeo kama ilivyoainishwa katika Mkataba wa Ruzuku. 

Katika Hafla hiyo wamehudhuria wadau mbalimbali Profesa James Mdoe, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mwenyekiti wa Bodi ya COSTECH Prof. Makenya Maboko, Kaimu Mkurugenzi wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Ladslaus Mnyone, Mkurugenzi, Idara ya Maendeleo ya Watu Lisa Sivertsen pamoja na Watafiti na Washirika wa Utafiti 

0/Post a Comment/Comments