Vyombo vya habari vimeombwa kufuata maadili ya kazi zao hasa katika kipindi hiki ambapo machafuko yanayoendelea kati Israel na Palestina .
Rai hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Balozi wa Palestina nchini Tanzania, Hamdi Mansour Abuali,wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya machafuko yanaendelea kati ya Israel na Palestina.
Aidha,Balozi Abuali amesema kwa sasa baadhi ya vyombo vya habari vya Magharibi vimekuwa vikiripoti habari mbaya kuhusu Palestina ikiwemo kuonesha habari za uongo kuhusu wapalestina
Balozi Abuali,amebainisha kuwa Raia wapalestina wanaonewa na kunyanyaswa ikiwemo kupoteza maisha ya raia wasikuwa na hatia kutoka na machafuko hayo.

Post a Comment