ELIMU YAHITAJIKA KWA WANANCHI KUHUSU KATIBA MPYA,DKT MAJINGE ATOA DARASA, AMSIFU RAIS SAMIA.


****"

IMEELEZWA kuwa ili iweze kupatikana katiba bora ambayo itakidhi matakwa ya Taifa, suala la elimu linahitajika kwa wananchi ili waweze kufahamu maana na umuhimu wa mchakato wa katiba mpya.

Rai hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Msaikososholojia na mtaalam wa Maendeleo ya Binadamu na Afya ya Akili Kinga, Dkt. Mayrose Majinge wakati akizungumza na waandishi kuhusu masuala ya Katiba ya nchi, Uzalendo na suala la kuongeza na kupunguza mamlaka ya Rais.

" Wananchi wanahaja ya kueleweshwa maana ya katiba. Katiba ni sheria mama inayosimamia misingi mikuu ya kisiasa na kuonesha madaraka na majukumu ya serikali hivyo wananchi waelimishwe wajue"Amesema Dkt. Majinge.

Aidha, Dkt. Majinge amesema nia ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha Taifa linapata katiba bora hivyo suala la elimu kwanza kwa wananchi alilosema Mhe. Rais lilikuwa la msingi.

Sanjari na hayo,Dkt. Majinge,ameshauri pia mchakato wa katiba mpya , ujikite katika kuimarisha Katiba ya kimapokeo (isiyoandikwa)lengo likiwa kupata katiba ya nchi iliyo madhubuti kwa vizazi na Vizazi .

Akizungumzia kuhusu uzalendo wa Taifa,Dkt. Majinge amesema "ili taifa liweze kupiga hatua kwenye maendeleo endelevu, watu wake wanapaswa kuwa wazalendo katika Taifa.

Kadhalika,Dkt. Majinge, ametoa maoni kwa watu wanaotaka Mamlaka ya Rais kupunguzwa na kupinga hoja hiyo kwa kusema ni kumpunguzia nguvu ya utiisho wa Rais kwa watu wake na hivyo kulipunguzia Taifa nguvu yake.

"haipaswi kumpungumzia mamlaka wala madaraka Rais bali iwe kuimarisha mamlaka "Amesema Dkt Majinge.

0/Post a Comment/Comments