MAFUNZO YA KUONGEZA UJUZI YALIVYOWANUFAISHA WANANCHI 49,000

Afisa habari wa Mradi wa Kuendeleza Ujuzi (SDF) Eliafile Solla, akizungumza katika kilele cha Juma la Elimu ya Watu Wazima ambalo maonesho yake kitaifa yanafanyika wilayani Kibaha mkoani Pwani,. 

Afisa habari wa Mradi wa Kuendeleza Ujuzi (SDF) Eliafile Solla, akizungumza na Mwananchi aliyefika katika banda lao katika kilele cha Juma la Elimu ya Watu Wazima ambalo maonesho yake kitaifa yanafanyika wilayani Kibaha mkoani Pwani, 

Mnufaika wa Mafunzo hayo  Esther Shebe, ambaye yeye ni mkulima wa Uyoga na msindikaji wa bidhaa za uyoga kionyesha zao la uyoga lililotayari kwa kuuzwa. 

Bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na Uyoga zilikuwepo kwenye banda la Mamlaka ya Elimu nchini Tanzania (TEA),. 

Mnufaika wa mafunzo ya kuongeza ujuzi ambaye yeye amejikita kwenye Usindikaji wa viungo vya chakula kutoka Iringa Mjini Geshom Mwinyi, akingumza katika kilele cha Juma la Elimu ya Watu Wazima ambalo maonesho yake kitaifa yanafanyika wilayani Kibaha mkoani Pwani. 

(PICHA ZOTE NA JAMES SALVATORY) 

                                 *******

Na James Salvatory


Mamlaka ya Elimu nchini Tanzania (TEA) imesema zaidi ya watanzania 49,000 nchi nzima wamenufaika na mafunzo ya Kuendeleza Ujuzi katika sekta sita za kipaumbele na kuleta tija katika ajira ikiwemo sekta ya Kilimo, Utalii na Huduma Ukarimu, Nishati, Ujenzi, tehama na Uchukuzi.

Mafunzo hayo yameweza kuleta tija kwa wanufaika kujiajiri wenyewe na kuwaajiri watu wengine na kuweza kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza wakati wa kilele cha Juma la Elimu ya Watu Wazima ambalo maonesho yake kitaifa yanafanyika wilayani Kibaha mkoani Pwani, afisa habari wa Mradi wa Kuendeleza Ujuzi (SDF) Eliafile Solla amesema kuwa mafunzo yalianza kutolewa tangu 2017 mpaka 2023 ambapo wengi wa wanufaika hao kwa sasa wamejiajiri na waliosalia wameajiriwa kutokana na mafunzo waliyoyapata.

Amesema kuwa mafunzo hayo yametolewa Tanzania Bara na Zanzibar ambapo Zanzibar kuna wanufaika 600 waliotoka katika kanya masikini ambao wamesajiliwa kwenye kanzi data ya Mpango wa kunusuru kaya masikini TASAF.

Aidha Bi Solla amewataka wanufaika wote waliopatiwa mafunzo hayo wasikae nyumbani wakati wana ujuzi tayari hivyo wathubutu kuanza kufanyia kazi ujuzi huo na elimu walioipata.

Kwa upande wake Mnufaika wa mafunzo ya kuendeleza ujuzi ambaye yeye amejikita kwenye Usindikaji wa viungo vya chakula kutoka Iringa Mjini Geshom Munyi, amesema amepata manufaa makubwa kutokana na mafunzo hayo licha ya kukabiliana na changamoto ya udogo wa mtaji.

“Wateja wamekuwa wengi lakini uwezo wa kuwahudumia ni mdogo kutokaa na mtaji kuwa mdogo hivyo kama nitawezeshwa mtaji naweza kuongeza uzalishaji na kuajiri watu wengi zaidi” amesema Munyi

Aidha amesema ujuzi huo umekuwa na manufaa makubwa kiasi cha kuamua kuacha kazi ya ualimu kwani alikuwa ameajiriwa na kuamua kujiari hali ambayo imemsaidia kupata kipato zaidi.

Naye Mnufaika Mwingine wa Mafunzo hayo Bi. Esther Shebe, ambaye yeye ni mkulima wa Uyoga na msindikaji wa bidhaa za uyoga anadai kuwa anakutana na changamoto kubwa ya vifaa na mtaji kuwa mdogo hivyo kuomba wadau na serikali kuwaunga mkono katika kazi zao za kila siku.

Mafunzo ya Kuendeleza Ujuzi yalikuwa yakitolewa na vyuo mbalimbali vyenye ithibati kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Maadhimisho ya “Juma la Elimu ya Watu Wazima” linatarajiwa kufikia tamati Ijumaa, Oktoba 13 mwaka huu huku idadi ya watu wazima wanaojua kusoma na kuandika ikitajwa kuongezeka.


0/Post a Comment/Comments