MARUFUKU WANANCHI KULALA GIZA KISA UMEME




Naibu waziri wa Nishati Judith Kapinga akizungumza na waandishi wa habari Mara baada ya ziara ya kukagua kituo cha uzalishaji umeme cha gesi kilichopo Tegeta, jijini Dar es salaam. 



Naibu waziri wa Nishati Judith Kapinga  akifanya ziara ya kukagua kituo cha uzalishaji umeme cha gesi kilichopo Tegeta, jijini Dar es salaam. 






Mitambo mbalimbali KATIKA kituo cha uzalishaji umeme cha gesi kilichopo Tegeta, jijini Dar es salaasalaam. 

(PICHA NA JAMES SALVATORE) 
"""""""""


Naibu waziri wa Nishati Judith Kapinga  amepiga marufuku wananchi kulala giza kisa kuna changamoto ya Transformers au ways umeanguka Huku Tanesco wapo wanachelewesha huduma hiyo kwa wananchi.

Ametoa agizo hilo kwa shirika la umeme Tanzania (TANESCO) Mara baada ya kukagua kituo cha uzalishaji umeme cha gesi kilichopo Tegeta, jijini Dar es salaam na kuwataka waimarishe huduma na kuondoa changamoto ndogo ndogo ambazo zinaweza kusababisha kero kwa wananchi.

“Ni kuhakikisha matengenezo ya mitambo ya lazima yanafanyika kwa wakati na muda mfupi ili kuendelea kuomarisha Hali ya upatikanaji wa umeme na panapotokea hitilafu basi hitilafu hizo zinafanyiwa kazi kwa haraka ili umeme uendelee kupatikana niwaelekeze Tanesco watanzania wanapopata changamoto ndogo ndogo za hitilafu za luku, transformers  au waya umekatika waimarishe mfumo wao wa utoaji huduma kwa wateja, hatutakubali wananchi walale giza kwa sababu tu transformer imeharibika halafu haijarekebishwa kwa wakati”, JUDITH KAPINGA-Naibu waziri wa Nishati.

Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa TANESCO mhandisi Isima Nyamhanga anasema shirika linaendeleza jitihada za kupunguza changamoto ya upatikanaji wa umeme.

“Upungufu kwenye mitambo yetu unaendelea kushuka , utakumbuka nilisema utakuwa unapungua kidogo kidogo kwa taarifa tulizonalo leo kutokana na jitihada tunazofanya upungufu upo takribani megawatt 300-350 ukilinganisha na hapo nyuma ambapo kulikuwa na upungufu wa megawatt 400”, MHANDISI ISIMA NYAMHANGA-Mkurugenzi Tanesco.


0/Post a Comment/Comments