MHE.MTINIKA ATAKA KASI UFUATILIAJI ELIMU YA WATU WAZIMA.


 .........................

Na:Shalua Mpanda-TMC

Kilele cha Maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu Wazima kiwilaya kimefanyika leo Oktoba 09,2023 ambapo Mstahiki meya wa manispaa hii Abdallah Mtinika.

Katika Maadhimisho hayo yaliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali za Msingi,Mhe.Mtinika amewaagiza wakuu wa Idara kutenga bajeti kwa ajili ya shughuli za Elimu ya Watu Wazima.

Pia amewataka wakuu hao wa Idara kuipa "uhai"Elimu hiyo kwa kuhamasisha,kuanzisha,kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa Programu mbalimbali za Elimu ya Watu Wazima.

"Naomba wananchi wenzangu kuzitumia fursa mbalimbali za Elimu ya Watu Wazima na walio nje ya mfumo rasmi kuondoa changamoto za ujinga,umaskini na maradhi ambazo bado tunazo".Alisisitiza Mhe.Mtinika

Kwa upande wake Afisa Elimu ya Watu Wazima Halmashauri ya manispaa ya Temeke Bi.Donasiana Njuu amesema,elimu nje ya mfumo rasmi inatoa fursa kwa watu kujiendeleza kutoka hatua ya chini kielimu hadi hatua za juu kupitia Programu zake mbalimbali .

Maadhimisho ya mwaka huu yenye kauli mbiu "Kukuza uwezo wa kusoma na kuandika kwa ulimwengu unaobadilika:Kujenga Misingi ya Jamii endelevu yenye amani",kitaifa yanafanyika katika mkoa wa Pwani.

0/Post a Comment/Comments