MIAKA 20 YA TCAA,MJADALA MKUBWA WAANDALIWA,MAJALIWA NDANI.



******

Mamlaka  ya Viwanja vya Ndege(TCAA) imeandaa mjadala wa wadau wa usafiri wa Anga kwa lengo la kuwakutanisha pamoja kujadili mafanikio na chagamoto mbalimbali zilizopo katika sekta hiyo.

Mjadala huo unatarajia kufanyika Octoba 30 katika ukumbi wa Mwalimu Julias Nyerere ambapo mgeni rasmi anatarajia kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa .

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam leo kuhusiana na Maadhimisho ya miaka 20 ya TCCA, Mwenyekiti wa Maadhimisho hayo Mellania Kasese  amesema kabla ya mjadala huo kutakuwa na  mbio za hisani ambazo zinatarajiwa kufanyika Octoba 29 katika Viwanja vya mlimani city ambapo mgeni rasmi anatarajia kuwa  wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila .

Aidha,Kasese amesemj mjadala huo utatoa nafasi kwa wadau wa sekta ya usafiri wa Anga kutoa chagamoto mbalimbali wanazokubana nazo.

"Octoba 5 mwaka huu Mkurugenzi Mtendaji wa  Mamlaka hii aliweza kuzindua Maadhimisho haya na kuweka  bayana  mafanikio na chagamoto katika miaka 20 ya Maadhimisho hayo hivyo hii ni Moja ya njia ya kukutana na wadau wa sekta hii kujadiliana mambo mbalimbali "amebainisha kuwa 

Kwa upande wa mbio za hisani ,amesemj  maandalizi ya mbio hizo tayari yamekamilika tayari  ambapo mbio hizo zitaanzia katika Viwanja vya mlimani city Jijini Dar es salaam.

Kadhalika,Kasese amesema  katika mbio hizo za hisani zitaanzia katika ruti ya   kilometa tano mpaka kumi  hivyo amewaomba watanzania kujitokeza kwa wingi.

"Shamra shamra za  Maadhimisho haya zimekuwa zikiendelea  yakiendelea lengo likiwa kuzungumzia mafanikio yaliopatikana katika miaka hiyo 20 mpaka sasa maandalizi yamekamilika vifaa vyote vimeishawasili na Octoba 30 kutakuwa na mjadala wa wasafiri wa Anga "Kasese

Pia Kasese amesema lengo ni kuu la mbio hizo ni kuinga  mkono  jamii iliyoko katika maeneo ya ukame ili iweze kupanda miti ya kutosha Ili kupunguza uhalibifu wa hali ya hewa.

Naye katibu wa Chama Cha riadhaa  mkoa wa Dar es salaam , Samweli Mwela amesema   tangu awali wamekuwa walishirikiana na TCAA katika  maandalizi ya mbio hizo wamekuwa walishirikiana vyema katika maandalizi kutokana na Chama hicho ndio limekuwa kikiusika katika mbio zote.

"Tumejiridhisha na kupima njia zote zitakazotumika katika mbio hizo Ili kuhakikisha zinakuwa katika Hali ya usalama"alisema alisema Mwela 


Huku akitoa wito kwa wadau wengine wanaofanya mbio za hisani kushirikiana na Chama hicho Ili kuweza kuepukana na chagamoto mbalimbali ambazo zinaweza kujitokeza.


 

0/Post a Comment/Comments