"""""""
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba, amepongeza hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuwawezesha na kuwainua vijana kupata fursa mbalimbali za ajiraa
Mshomba amesema hayo tarehe 13 Oktoba 2023, wakati alipotembelea Maonesho ya Wiki ya Vijana yanayofanyika katika Stendi ya Zamani, Babati Mkoani Manyara, akiwa amefuatana na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Omar Mziya na Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani, Godfrey Ngonyani.
Amempongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kazi nzuri anayoifanya katika kuhakikisha vijana wanashiriki shughuli mbalimbali za kiuchumi.
"Namtakia kila la heri Mheshimiwa Rais katika kuhakikisha malengo yake aliyonayo kwa vijana na Watanzania kwa ujumla yanatimia na nchi yetu inapiga hatua za maendeleo," amesema Mshomba.
Mshomba amesema vijana ni wadau muhimu kwa NSSF kwa sababu ndio nguvu kazi kubwa ya Taifa, na pia ni wanachama wa Mfuko, ambapo baadhi wanachangia kupitia sekta binafsi na wengine wanachangia kupitia sekta isiyo rasmi.
"Ushiriki wa NSSF katika Maonesho haya ya Wiki ya Vijana umewalenga moja kwa moja vijana ambao tunawapatia elimu ya hifadhi ya jamii ili waweze kujiunga na kujiwekea akiba kwa maisha yao ya sasa na ya baadaye," amesema Mshomba.


Post a Comment