*******
TAASISI ya Saratani ya Ocean road imesema itaendelea kuwekeza nguvu kwa tiba shufaa ili kuwasaidia wagonjwa wanaougua magonjwa ya Muda mrefu ikiwemo saratani kwenye Matibabu.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi mtendaji wa Ocean Road,Julius Mwaisalage,wakati maazimisho ya tiba shufaa Duniani ambayo imekuwa ikianzimishwa kila jumamosi ya wiki ya pili ya mwezi oktoba.
Mwaisalage,amesema dhamira ya serikali ya awamu ya tano ni kuendelea kuhamasisha hospitali mbalimbali nchini Tanzania ikiwemo kutoa tiba shufaa huku jukumu la tiba hiyo ni kumfanya mgonjwa wa Saratani asiwe na maumivu mengine
Aidha,Mwaisalage amefafanua kwa kusema kuwa Tiba shufaa ni tiba inayolenga kuimarisha na kuboresha maisha ya mgonjwa na familia yake kwa wagonjwa wanaoumwa magonjwa ya muda mrefu.
"Tiba hii haitolewi na watu wa huduma za afya tu bali ni muunganiko wa wataalamu mbali mbali ikiwemo watu wa kiimani ,lishe ,wataalamu wa saikolojia pamoja na ustawi wa jamii ili kusaidia afya na akili ya mgonjwa"Amesema Mwaisalage.
Kwa upande wake,Faraja Kiwanga,amesema taasisi ya ocean road imekuwa ikipokea wagonjwa ambao tayari wapo katika hatua kubwa inayompelekea kupata hali ya msongo wa mawazo na kubainisha kuwa tiba shufa ambayo inamsaidia mgonjwa kupata faraja na tiba hii inaanza kipindi ambacho mgonjwa kagundulika kuwa ana ugonjwa huo ili kuboresha maisha ya mgonjwa na familia yake.


Post a Comment