TASAC YATOA MCHANGO WA 43 BILIONI SERIKALINI


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Nelson Mlali akizngumza na wahariri wa vyombo vya Habari katika semina iliyoandaliwa na msajili wa hazina  Jijini Dar es Salaam. 



Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Deodatus Balile akizungumza kwa niaba ya wahariri na waandishi wa habari.




Waandishi wa habari na wahariri wa vyombo mbalimbali wakiendelea na kikao na Shirika la uwakala wa meli Tanzania (TASAC). 







Wahariri wa vyombo vya Habari wakiuliza Maswali Viongozi wa TASAC, katika semina iliyoandaliwa na msajili wa hazina ikifanyika  Jijini Dar es Salaam.
Wahariri wa vyombo vya Habari mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa TASAC. 

(PICHA ZOTE NA JAMES SALVATORY) 

*******
Na Mwandishi Wetu

Shirika la uwakala wa meli Tanzania (TASAC) limefanikiwa 
kuchangia mchango katika mfuko wa serikali kutoka sh bilioni 9 mwaka 2018 hadi sh bilioni 43 kwa mwaka 2023.

Akizungumza na wahariri wa vyombo vya Habari katika semina iliyoandaliwa na msajili wa hazina  Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Nelson Mlali ameeleza kuwa mafanikio hayo yamesababishwa kutokana na Usikivu wa Serikali inayoongozwa na Rais
Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kupokea ushauri
mbalimbali wa kitaalam na kutoa
maelekezo sahihi kupitia Wizara ya Uchukuzi lakini pia Kuzingatia miongozo mbalimbali inayotolewa na
Serikali pamoja na kamati za Bunge.

Aidha amesema wamefanikiwa Kuongeza idadi ya watoa huduma wanaodhibitiwa na TASAC kwa
 maana ya idadi ya leseni na vyeti vya usajili vilivyotolewa lakini pia kuongezeka kwa idadi ya vyeti kwa mabaharia waliokidhi masharti.

Amesema wamefanikiwa Kuongeza idadi ya watoa huduma wanaodhibitiwa na TASAC kwa maana ya idadi ya leseni na vyeti vya usajili vilivyotolewa lakini pia kuongezeka kwa idadi ya vyeti kwa mabaharia waliokidhi masharti.

Pia amesema  "Mafanikio yanayopatikana ni kuongezeka kwa idadi ya leseni za vyombo vidogo, Kuongezeka kwa idadi ya kaguzi za meli za kigeni lakini pia Kuongezeka kwa mchango katika mfuko mkuu wa Serikali"

Pia Mlali amesema wamefanikiwa kuimarisha udhibiti wa huduma za bandari baada ya urasimishaji wa maeneo 20 ya
 kibandari katika mwambao wa bahari na
 maziwa

Kwa upande wa Changamoto, Mlali ametaja shirika kukabiliwa na changamoto kuu mbili ikiwemo Mabadiliko ya haraka ya teknolojia katika
sekta na mahitaji makubwa ya mifumo ya TEHAMA na uhaba wa wataalamu wa ndani katikamajini baadhi ya taaluma hasa wakaguzi wa
usalama wa vyombo vya usafiri majini.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Deodatus Balile ameipongeza TASAC kwa utendaji wake na kuwashauri kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya fursa mbali mbali zinazopatikana katika sekta ya usafiri wa majini hapa nchini.

Shirika la uwakala wa Meli Tanzania TASAC lilianzishwa rasmi mwaka 2018 likiwa na jukumu kuu la kusimamia usafiri kwa njia ya maji.

0/Post a Comment/Comments