Katibu Mtendaji wa TCU Charles Kihampa wakati akizungumza na wandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakimsikiliza Katibu Mtendaji wa TCU Charles Kihampa mapema leo jijini Dar es Salaam.
*******
Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) imefungua awamu ya nne na ya mwisho ya udahili iliyoanza leo na Waombaji ambao hawakuweza kutuma maombi au hawakufanikiwa kudahiliwa katika awamu zilizopita kutokana na sababu mbalimbali watumie fursa hiyo kwa kutuma kwa usahihi maombi yao ya kwenye vyuo wanavyovipenda.
Hayo yamebainishwa na Katibu Mtendaji wa TCU Charles Kihampa wakati akizungumza na wandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam ambapo amesema udahili katika awamu zote tatu kwa ngazi ya shahada ya kwanza katika Taasisi ya elimu ya juu nchini kwa mwaka wa masomo 2023/24 umekamilika na majina ya waliodahiliwa katika awamu ya tatu yanatangazwa na vyuo husika
Aidha amesema Dirisha hilo litadumu kwa siku tano likiwa ni nafasi ya mwisho kwa wanafunzi wote wenye matumaini ya kujiunga na vyuo vikuu mwaka huu.
Amesema kwa mwaka huu wa masomo vyuo vikuu vina jumla ya nafasi 187,000 na hadi sasa waliodahiliwa ni 130,116 hivyo bado kuna nafasi ambazo ziko wazi.
Kufunguliwa kwa dirisha hilo kumeenda sambamba na maelekezo kwa wanafunzi waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja kujithibitisha katika chuo kimojawapo ili kuacha wazi nafasi katika vyuo vingine kwa ajili ya waombaji wengine.






Post a Comment