TIB YATOA MIKOPO YA BILIONI 980

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIB, Lilian Mbassy akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari leo Jumatatu Oktoba 16,2023

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania ( TEF), Deodatus Balile, akitoa salama kwa niaba ya wahariri wa vyombo vya habari nchini. 





Wahariri na Waandishi wa vyombo vya habari nchini wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIB, Lilian Mbassy akitoa wasilisho lake mapema Leo Jijini Dar es salaam. 

       (PICHA ZOTE NA JAMES SALVATORY) 
                               ********

Na James Salvatory

BENKI  ya Maendeleo Tanzania (TIB), imetumia jumla ya Sh980.7 bilioni kama mkopo ili kuwekeza katika miradi mbalimbali ikiwamo ya kilimo, utalii, madini na uchakataji pamoja na ujenzi wa majengo.

Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari leo Jumatatu Oktoba 16,2023 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIB, Lilian Mbassy amesema asilimia 93 ya mkopo huo imetolewa kwa mirai ya sekta binafsi na saba pekee ni ya umma.

“Asilimia 80 ya mirada ni ya muda mrefu kuanzia miaka mitano na kuendelea ambako Kilimo na usindikaji inaongoza kwa kupewa Sh334.6 sawa na asilimia 34 ya fedha zote ikifuatiwa na Madini na uchakataji iliyopewa Sh 205 milioni wakati sekta ya utalii ilipewa Sh 154 milioni.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Lilian, Jumla ya miradi 253 imepatikana katika sekta ya kilimo na usindikaji iliyotekelezwa katika mikoa 23 na wilaya 76 zimenufaika.

“Zaidi ya wananchi 10,230 wamepata ajira katika sekta ya kilimo, taasisi za kifedha 12, saccoss 78 na kampuni 128 zimekopeshwa.”

Alisema kwa upande wa uwekezaji wa sekta ya majiji jumla ya mirada 66 imekopeshwa huku Mamlaka ya za Maji ikipata sita, Jumuiya za Watumiaji Maji Vijjjini 60 ambako kiasi cha Sh14.9 bilioni kiliwekezwa katika ya Maji na Ustawi wa Mazingira katika mikoa ya Iringa. Dodoma, Singida, Shinyanga, Tanga, Mtwara, Iringa, Morogoro na Ruvuma.

0/Post a Comment/Comments