Mwenyekiti wa Bima kutoka nchini Kenya, Godfrey Kiptum, akizungumza na waadishi wa habari Mara baada ya Mkutano wa Makashna na viongozi wa Mamlaka zinazohusika na usimamizi wa Bima katika Jumuhiya za Afrika Mashariki waliokutana kwa siku Tano kujadili njia Bora ya kuendeleza Sekta ya Bima katika nchi hizo. *********
Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini Tanzania TIRA, Dkt. Baghayo Saqware amewataka watoa huduma wote kuendelea kubuni huduma sahihi kwa wananchi huku watumiaji kuendelea kununua bidhaa na huduma za Bima kwaajili ya kujikinga na matukio mbalimbali.
Dkt Saqware ametoa Wito huo jijini Dar es salaam katika Mkutano wa Makashna na viongozi wa Mamlaka zinazohusika na usimamizi wa Bima katika Jumuhiya za Afrika Mashariki waliokutana kwa siku Tano kujadili njia Bora ya kuendeleza Sekta ya Bima katika nchi hizo ikiwa ni pamoja na kuona namna ya kuwawezesha raia wake kuwa na mwitikio mkubwa wa matumizi ya Bima.
Amesema Huduma hizo zinatoka fursa za uwekezaji hivyo wananchi watembelee Makampuni ili kuona namna ya kununua bidhaa za Bima.
Aidha mesema kwenye mpango wa kitaifa wa fedha wanahitajika kuwa na watanzania zaidi ya asilimia 50 ambao wanatakiwa kutumia huduma na bidhaa za Bima.
Hata hivyo amesema Nchi za Jumuiya ya Afrika mashariki-EAC zimedhamiria kuweka mpango mkakati wa kuendeleza soko la Bima na kukuza uelewa wa Bima kwa wananchi wa nchi hizo.
Mpango huo wamekubaliana kuuzindua mwaka 2024 nchini Kenya ambapo Kamishna wa Kenya atakuwa Mwenyeji wa Mkutano huo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bima kutoka nchini Kenya, Godfrey Kiptum amesema changamoto kubwa iliyopo katika nchi za Afrika Mashariki ni uwepo wa idadi ndogo ya watu wanaotumia Bima hivyo kuwataka wananchi wote wa Nchi hizo kutumia Bima za Maisha.


Post a Comment