TRA YAWATAKA WALIPAKODI KUTEKELEZA MATAKWA YA KISHERIA KATIKA ULIPAJI KODI.


..................

 Timothy Marko

Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imewataka walipa kodi wakubwa kutekeleza matakwa ya kisheria ya ulipaji kodi .
Akizungumza katika kikao kilicho wakutanisha walipakodi wa wakubwa nchini jijini Dar es salaam Kamishina wa Mamlaka ya  Mapato nchini TRA  Alphayo kidata   amesema  sekta ya umma  nikichocheo cha maendeleo ya kiuchumi nakuzitakataasisi hizo kulipa kodi zao kwa wakati.

"Uhakika wa wamakusanyo ya kodi katika taasisi za umma na binafsi ndio chanzo cha Mapato ya.     Serikali,Mapato haya ndio hutumika utekelezaji wa miradi ya Maendeleo"Alisema Kamishina Alphayo kidata.
                        
Kamisha kidata alisema Ulipaji wa kodi stahiki nikwamujibu wa sheria ikijumuisha sekta binafsi na uuma.
Alisema Taasisi za  Umma ni Muhimu kulipa kodi nasuala hilo ni lazima nasio la hiyari.
"Naziomba taasisiza umma zishirikiane na taasisi za binafs katika kukuza uelewa wa ulipaji kodi".Aliongeza Alphayo kidata.

Katika hatua nyingine Kamishina wa Walipa kodi wa Wakubwa Thomas Muhoja amesema lengo lamkutano huo unalenga kuzungumzia mabadiliko ya kodi ambayo yatatumika katika mwaka ujao wa fedha.
Alisema TRA inawakumbusha walipakodi kutekekeleza magizo ya mamlaka hiyo ilikuweza kuchangia  maendeleo ya taifa.
"TRAtuna wakumbusha kutimiza maelekezo ilikuchangia maendeleo ya nchi".Alisema Muhoja.

 

0/Post a Comment/Comments