Na:Shalua Mpanda -TMC
Wito
umetolewa kwa wadau wa elimu nchini kutumia changamoto iliyopo ya upungufu wa
walimu kubuni mbinu za kisasa kukabiliana na changamoto hiyo.
Wito
huo umetolewa leo na mkuu wa wilaya ya
Temeke mheshimiwa Sixtus Mapunda wakati wa sherehe za mahafali ya kidato cha
nne katika shule ya Sekondari Kijichi.
Mhe.Mapunda
amesema Serikali inajitahidi kuajiri walimu
lakini haiwezi kumaliza changamoto hii hivyo ni wakati muafaka sasa kuanza kutumia teknolojia
kukabiliana na jambo hili.
"Tumieni
walimu wachache waliopo lakini kwa mfumo wa kisasa,Dunia hivi Sasa mwalimu
anaweza kuwa darasani lakini akamfundisha mtoto akiwa hapa...kinachotakiwa hapa
ni 'internet' na screen
kubwa".Alisema Mkuu huyo wa Wilaya.
Awali
akimkaribisha mkuu wa Wilaya,mwalimu mkuu wa Shule hiyo Bi.Catherine Mdachi
alisema wamejipanga kufanya vizuri katika mitihani ya kidato cha nne mwaka huu
kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na walimu.
Katika
hatua nyingine Mhe.Mapunda amewashukuru walimu wanaojitolea katika Shule hiyo
ambapo ameahidi kukutana na walimu hao ofisini kwake kuzungumza nao kama
motisha kwa kazi wanayofanya.
Serikali
ya awamu ya sita chini ya Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imekuwa ikiipa
kipaumbele sekta ya elimu kwa kutoa kiasi kikubwa cha fedha katika kuboresha
miundombinu ya elimu.


.jpeg)

.jpeg)
Post a Comment