********
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu profesa Joyce Ndalichako amewataka waajiri nchini kuweka mifumo ambayo ni endelevu itakayohakikisha kwamba wafanayakazi wanapata fursa ya kuimarisha afya zao pamoja na kufanya kazi Ili kupunguza Magonjwa na Vifo mahali pa kazi ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya ugonjwa wa Afya akili Duniani.
Amesema Kumekuwa na matukio mbalimbali yanayotokana na wengi wao kuwa na msongo wa Mawazo katika Maeneo yao ya kazi na kupelekea kupoteza Maisha na hivyo waajiri wachukue hatua za makusudi kupunguza adha hiyo.
Profesa Ndalichako
ameyasema leo jijini Dar es salaam,katika Bonanza ya waajiri iliyowakutanisha waajiriwa kutoka katika sekta mmbalimbali ambayo imeandaliwa na chama cha waajiri Tanzania (ATE), ikiwa na lengo ni kuendelea kuimarisha afya zao na kutenda kazi zao kwa ufanisi na kuongeza uzalishaji.
Aidha amesema Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kazi na kuweka mifumo thabiti ya kuhakikisha kuwa nguvukazi ya Taifa
Awali akifanya utambulisho Mtendaji Mkuu wa Chama cha waajiri Tanzania ATE Suzanne Ndomba -Doran ndomba amesema Bonanza hiyo imelenga kuimarisha afya ya kwa wafanyakazi wa Ili watende kazi Kwa ufanisi na kupunguza migogoro isiyokuwa ya lazima



Post a Comment