Wanafunzi 250 wa darasa la nne llala wapewa chakula bure na Mwenyekiti Bechina

........,......

Na Herishaban@gmail.com (Ilala)

Serikali ya Mtaa Kalume imetoa chakula bure cha wanafunzi wa 250  wa  darasa la nne leo wanaofanya mtihani wa kuingia darasa la tano wa  msingi shule ya msingi Ilala Boma na Mkoani .

Akizungumza wakati wa kugawa chakula kwa wanafunzi wa shule ya Ilala Boma Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Kalume Hajji Bechina, alisema utaratibu wa kurisha chakula bure kwa wanafunzi    kwa shule ya Ilala Boma na Mkoani ni endelevu kila mwaka .

"Serikali ya mtaa Kalume Ilala kwa kushirikiana na chama cha Mapinduzi CCM tawi la Shauri moyo tumeweka utaratibu wetu wa kulisha chakula bure shule za kata ya Ilala ,Ilala Boma na Mkoani  kugawa chakula bure kila mwaka katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan "alisema Bechina 

Mwenyekiti Bechina alisema  Serikal  ya Mtaa Kalume  imewapunguzia Wazazi mzigo watoto wao siku mbili za mitihani wanakula chakula bure kinachogharamia na Ofisi ya  Serikali ya Mtaa kuanzia chai asubuhi na chakula cha mchana  kila mwaka.

Alisema pia wasimamizi 25 wa shule hizo mbili wanaosimamia mitihani pia wanakula chakula bure kinachoandaliwa na Serikali ya Mtaa Kalume. 

MWENYEKITI BECHINA aliwatakia khery   darasa la nne  wafanye vizuri mitihani yao kwa siku hizo  mbili.

Alisema Serikali ya Mtaa Kalume inaunga mkono sera ya Serikali ya elimu bure na kuwawezesha wanafunzi chakula na kuweka mazingira bora ya shule za Ilala Boma na Mkoni Wilayani Ilala.

0/Post a Comment/Comments