Mkurugenzi Mkuu Wa Bodi ya Mikop ya Elimu ya juu nchini (HESLB), Abdul-Razaq Badru akizungumza jijini Dar es Salaam, katika kikao kazi kati ya bodi hiyo na wahariri pamoja na waandishi Wa habari. Afisa uhusiano na Mawasiliano kutoka Ofisi ya Msajili Wa Hazina, Sabato Kosuri, akiongoza kikao kazi na kati ya Bodi ya mikopo ya Elimu ya juu nchini (HESLB),
Bodi ya mikopo ya Elimu ya juu nchini (HESLB), imesema, tangu kuanzishwa kwake Ukwasi umefikia zaidi ya shilingi trillioni 7.2 ambazo zimekwenda kwa wanufaika 750,000 nchini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, katika kikao kazi kati ya bodi hiyo na wahariri pamoja na waandishi Wa habari chini ya utaratibu Wa ofisi ya Msajili Wa Hazina, Mkurugenzi Mkuu Wa (HESLB), Abdul-Razaq Badru amesema kufikia septemba mwaka huu kiasi cha mikopo ambacho kimekusanywa kinakadiriwa kufikia shilingi trillioni 1.3 kutoka kwa wakopaji zaidi ya 230,000.
Aidha amesema kiasi cha shilingi billioni 700 cha mikopo hiyo zimeiva lakini hazijakusanywa.
Pia, amesema wapo katika hatua za kushirikiana na wadau mbalimbali ili kufanikisha ukusanyaji Wa mikopo hiyo ikiwemo kuunganisha mifumo yao na hifadhi za Jamie na mamlaka ya mapato Tanzania kuendelea kutoa Elimu.
Amesema kwa sasa mifumo yao imeunganishwa na mifumo mama ya Taifa kwa ajili ya kuongeza ufanisi na utekelezaji Wa majukumu yao.
Kwa upande wake afisa uhusiano na Mawasiliano kutoka Ofisi ya Msajili Wa Hazina, Sabato Kosuri, amesema kuwa wanasimamia maslahi ya serikali kwenye Taasisi za umma.











Post a Comment