Naibu
Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), akifungua Mkutano wa
Maadhimisho ya Miaka 15 ya Mradi wa Utafiti wa Kupima Hali ya Maisha
zinazojumuisha Tafiti za Kilimo Katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara,
uliofanyika katika Hoteli ya Delta jijini Dar es salaam. Mkutano huo wa siku
mbili umehudhuriwa na watalamu wa uchumi, sera na watafiti kutoka nchi
mbalimbali za Kusini mwa Jangwa la Sahara ambapo matokeo ya baadhi ya tafiti
zilizofanyika chini ya mradi huo zinawasilishwa.
Mtakwimu
Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa, akizungumza wakati akimkaribisha Naibu
Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), kufungua Mkutano wa Maadhimisho
ya Miaka 15 ya Mradi wa Utafiti wa Kupima Hali ya Maisha zinazojumuisha Tafiti
za Kilimo Katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, uliofanyika katika Hoteli
ya Delta jijini Dar es salaam. Mkutano huo wa siku mbili umehudhuriwa na
watalamu wa uchumi, sera na watafiti kutoka nchi mbalimbali za Kusini mwa
Jangwa la Sahara ambapo matokeo ya baadhi ya tafiti zilizofanyika chini ya
mradi huo zinawasilishwa.
Naibu
Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) (wapili kulia), akifuatilia mada
iliokuwa ikitolewa na Meneja Miradi kutoka Benki ya Dunia, Bw. Gero Carletto
(hayupo pichani), wakati wa Mkutano wa Maadhimisho ya Miaka 15 ya Mradi wa
Utafiti wa Kupima Hali ya Maisha zinazojumuisha Tafiti za Kilimo Katika nchi za
Kusini mwa Jangwa la Sahara, unaofanyika katika Hoteli ya Delta jijini Dar es
salaam. Mkutano huo wa siku mbili umehudhuriwa na watalamu wa uchumi, sera na
watafiti kutoka nchi mbalimbali za Kusini mwa Jangwa la Sahara ambapo matokeo
ya baadhi ya tafiti zilizofanyika chini ya mradi huo zinawasilishwa.
Baadhi ya
wataalamu wa uchumi, sera na utafiti, wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri wa
Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), wakati akifungua Mkutano wa Maadhimisho
ya Miaka 15 ya Mradi wa Utafiti wa Kupima Hali ya Maisha zinazojumuisha Tafiti
za Kilimo Katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, unaofanyika katika Hoteli
ya Delta jijini Dar es salaam. Mkutano huo wa siku mbili umehudhuriwa na
watalamu wa uchumi, sera na watafiti kutoka nchi mbalimbali za Kusini mwa
Jangwa la Sahara ambapo matokeo ya baadhi ya tafiti zilizofanyika chini ya
mradi huo zinawasilishwa.
Kamisaa wa
Sensa ya Watu na Makazi, Mhe. Anna Makinda, akizungumza jambo wakati wa Mkutano
wa Maadhimisho ya Miaka 15 ya Mradi wa Utafiti wa Kupima Hali ya Maisha
zinazojumuisha Tafiti za Kilimo Katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara,
unaofanyika katika Hoteli ya Delta jijini Dar es salaam. Mkutano huo wa siku mbili
umehudhuriwa na watalamu wa uchumi, sera na watafiti kutoka nchi mbalimbali za
Kusini mwa Jangwa la Sahara ambapo matokeo ya baadhi ya tafiti zilizofanyika
chini ya mradi huo zinawasilishwa.Na. Josephine Majura na Joseph Mahumi, WF, Dar es Salaam
Tanzania imekuwa kwenye kiwango kizuri cha upatikanaji wa chakula kutokana na kuwepo kwa takwimu sahihi za hali ya Maisha katika kaya, hali iliyopolekea kiwango cha umasikini wa chakula kushuka nchini.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), wakati akifungua Mkutano wa Maadhimisho ya Miaka 15 ya Mradi wa Utafiti wa Kupima Hali ya Maisha zinazojumuisha Tafiti za Kilimo Katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara (Living Standards Measurement Study-Intergrated Survey on Agriculture (LSMS-ISA), katika Hoteli ya Delta, jijini Dar es Salaam.
Amesema Programu hiyo ya utafiti iliyoanza 2008 ambayo ilifadhiliwa na Benki ya Dunia imeweka alama sio tu katika uzalishaji wa takwimu muhimu za hali ya maisha katika kaya bali pia takwimu zilizozalishwa zimekuwa nyenzo muhimu za kutathmini sera na programu zinazotekelezwa na Serikali, taasisi binafsi na wadau wa maendeleo.
“Kiwango cha umasikini kwa sasa kimepungua hasa umasikini wa upatikanaji wa chakula, chakula kipo kwa wingi cha kutosha ambapo sisi watanzania leo tunalisha mpaka nchi jirani” amesema Chande
Kwa upande wake Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt Albina Chuwa, amesema miaka 15 ya mradi huo umeleta mafanikio makubwa nchini na barani Afrika kwa ujumla.
“Wakati utafiti unaanza 2008 katika Bara la Afrika nchi nyingi zilikua zinafanya utafiti kwa kutumia karatasi lakini sasa teknolojia imekuwa na sasa utafiti unafanywa kwa kutumia vishkwambi” amesema Dkt. Chuwa.
Naye, Meneja Miradi kutoka Benki ya Dunia, Bw. Gero Carletto, ameipongeza Tanzania kwa kuendelea kutoa ushirikiano katika programu hiyo na juhudi zinazochukuliwa na Serikali katika kupunguza umasikini wa chakula.
“ Kumekuwa na maendeleo makubwa sio tu katika kupunguza umaskini bali pia katika viashiria vingine vingi. Jopo la kitaifa la utafiti, limekuwa makini katika kuelewa vyema mienendo ya umaskini”. Bw. Carletto
Naye, Kamisaa wa Sensa, Mhe. Anna Makinda, amewataka watafiti kurudisha tafiti hizo kwa wananchi kwa maana wao ndio wahusika wakuu.
Amesema utafiti huu umefanikiwa kwa sababu umeweza kumfikia mtu mmoja mmoja na kuelezea ukweli kuhusu maisha yake jambo ambalo si rahisi.
“Hawa wataalam wa takwimu tunasema sasa wakati umefika utafiti wao uenze kuwatumikia hawa wananchi lakini pia utasaidia utendaji wa serikali katika kuwahudumia wananchi wake” amesema Makinda.
Mkutano
huo wa siku mbili umehudhuriwa na watalamu wa uchumi, sera na watafiti kutoka
nchi mbalimbali za Kusini mwa Jangwa la Sahara ambapo matokeo ya baadhi ya
tafiti zilizofanyika chini ya mradi huo zinawasilishwa.
Meneja
Miradi kutoka Benki ya Dunia, Bw. Gero Carletto, akizungumza wakati wa Mkutano
wa Maadhimisho ya Miaka 15 ya Mradi wa Utafiti wa Kupima Hali ya Maisha
zinazojumuisha Tafiti za Kilimo Katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara,
ambao umefunguliwa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb),
katika Hoteli ya Delta jijini Dar es salaam. Mkutano huo wa siku mbili
umehudhuriwa na watalamu wa uchumi, sera na watafiti kutoka nchi mbalimbali za
Kusini mwa Jangwa la Sahara ambapo matokeo ya baadhi ya tafiti zilizofanyika
chini ya mradi huo zinawasilishwa.
Naibu
Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) (wa sita kushoto), Meneja Miradi
kutoka Benki ya Dunia, Bw. Gero Carletto (wa tano kulia), Mtakwimu Mkuu wa
Serikali, Dkt. Albina Chuwa (wa tano kushoto), Kamisaa wa Sensa ya Watu na
Makazi, Mhe. Anna Makinda (wa sita kulia) na Mtakwimu Mkuu wa Serikali –
Zanzibar, Bw. Salum Kassim Ali, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi
kutoka Benki ya Dunia na Serikali, baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Maadhimisho
ya Miaka 15 ya Mradi wa Utafiti wa Kupima Hali ya Maisha zinazojumuisha Tafiti
za Kilimo Katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, ambao umefunguliwa na
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), katika Hoteli ya Delta
jijini Dar es salaam. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar es Salaam
Post a Comment