HALMASHAURI YA JIJI DAR IMEPATA FURSA UPIMAJI MJI (LTIP )

..........................

Na HERI SHAABAN( ILALA )

Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam imepata fursa ya uboreshaji umiliki ardhi upya (LTIP)katika halmashauri 200 nchini Tanzania. 

Mkakati Maalum wa uboreshaji umiliki ardhi umepata Baraka na Baraza la Halmashauri ya jiji hilo madiwani wa Ilala wamepitisha mradi huo ambao utasimamiwa na Serikali moja kwa moja na wananchi watapewa hati zao siku hiyo hiyo.

Akizungumza katika Baraza la Madiwani Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano Arnatoglou Meya wa jiji hilo Omary Kumbilamoto, kwa niaba ya madiwani wa Ilala walipitisha mpango huo wa Serikali. 

Meya Kumbilamoto alisema yeye na watendaji wa Halmashauri na madiwani wa Ilala wamepata elimu ya kutosha kuhusiana na mradi wa Serikali wa kuboresha umiliki wa ardhi nchini LTIP.

Kwa upande wake Paul Samwel Kitosi ,kutoka Timu ya Uratibu Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Umiliki za Ardhi alisema masuala ya urasimishaji baadhi ya mitaa kazi imeenda sawa baadhi ya mitaa kazi aikwenda sawa ambapo baadhi ya wananchi hawadhidi elfu 40 walipatiwa hati.

Paul alisema mradi huu utapita kila wilaya ambapo alisema kwa sasa pesa za kulipa kampuni akuna badala yake wataalam wa Serikali ndio watasimamia mpango huo na jiji la Dar es Salaam linaenda kunufaika baada ya wananchi kujisajili mradi huo utaongeza mihamara. 

Alisema mradi utapanga na kumilikisha viwanja milioni mbili na vijijini ni laki tano mfumo wa kidigitali utatumika kila mkoa watajenga ofisi za ardhi katika mikoa 25.

"SERA ya mfumo ya kisheria mradi unatekekeza ilani ya uchaguzi ya Serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ambapo hati milioni 2.6 zitatolewa vijijini "alisema Paul 

Alisema Halmashauri ya jiji ni Halmashauri kubwa watapanga mji na kupima upya ambapo mradi utafika kila sehemu maeneo yaliopangwa ambapo bado kupimwa kutapimwa .

Mpima Ardhi wa Halmashauri ya jiji Lugano Mwambaluma alisema lengo la mradi huo kukwamua mradi wa urasimishaji ambayo imekwama ,ambapo pia mradi huo utasimamia pia kutatua migogoro mbalimbali ya ardhi na kutanua wigo wa walipa kodi 

Afisa Lugano alisema mkakati wa Ilala watu kumiliki ardhi na kutatua migogoro mbalimbali ya ardhi dhamira ya mradi huo umelenga Jimbo la Ukonga na Segerea wilayani Ilala ambapo maeneo hayo wananchi elimu ndogo ambapo usimamizi na utekelezaji wa mradi katika halmashauri ya jiji mradi huo utasimamiwa na halmashauri ya jiji. 

Alitaja maeneo ya mradi huo Viwege ,Kimanga, Magole A,Magole,TABATA, kisukuru,Ulongoni,Bonyokwa ,Kifuru na Nguvu Mpya

0/Post a Comment/Comments