MAHAKAMA SITA KUJENGWA TANZANIA NDANI YA MIEZI TISA


                             ******

Mahakama  kwa kushirikiana na kampuni nne imesaini mikataba  yenye thamani ya shilingi bilioni 49  yenye lengo la  kujenga  ujenzi wa vituo sita  Jumuishi vya kutoa huduma ya mahakama katika mikoa mbalimbali nchini. 

Akizungumza wakati wa kutiliana Saini na makampuni hayo mapema leo jijini Dar es salaam,Mtendaji Mkuu wa mahakama ya Tanzania  Prof. Elisante Ole Gabriel amesema Mikoa hiyo ni pamoja na Njombe,Katavi ,Geita,Simiyu,Songea na Songwe. 

Ameongezea kuwa ana imani kuwa wakandarasi hao waliopewa kazi hiyo watafanya kazi kwa uweledi na kwa muda waliowekewa kwa miezi tisa

Aidha amesema mahakama haitosita kumchukulia hatua mkandarasi yeyote atakayekuwa kikwazo katika kufanikisha malengo hayo. 


Naye Mkuu wa kitengo cha maboresho ya mahakama Jaji Angelo Rumisha  amesema  Ujenzi huo wa vituo jumuishi vya kutoa huduma ya mahakama ni wa awamu hivyo bado serikali inaendelea na mchakato wa kujenga vituo vingine malengo ni vituo 14.

Kwa upande wake miongoni mwa wawakilishi wa waliosaini mkataba huo  Injinia Kapinga S.Kapinga Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Azhar Construction amesema wameahidi serikali na wananchi hawatowaangusha katika ujenzi huo. 





0/Post a Comment/Comments