Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko
akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Msimbati wilayani Mtwara, Mkoa wa
Mtwara akiwa njiani mara baada ya kukagua visima vya kuzalisha mitambo ya
kuchakata Gesi ya Mnazi Bay
Wananchi wa Kijiji cha Msimbati wilayani Mtwara, Mkoa wa
Mtwara wakimsikiliza Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe.
Dkt. Doto Biteko
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko
akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Msimbati wilayani Mtwara, Mkoa wa
Mtwara akiwa njiani mara baada ya kukagua visima vya kuzalisha mitambo ya
kuchakata Gesi ya Mnazi Bay.Msimbati - Mtwara
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe.
Dkt. Doto Biteko ameagiza kuondolewa kwa Meneja Mawasiliano wa Shirika la
Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kutokana na kushindwa kutoa taarifa
mbalimbali na kutofanya mikutano na wananchi wanaozunguka miradi ya Gesi Asilia
ikiwemo dharura zinazotokea katika Mkuza wa Bomba la Gesi.
Dkt. Biteko ametoa maagizo hayo tarehe 14
Novemba, 2023 wakati aliposimama katika Kijiji cha Msimbati wilayani Mtwara,
Mkoa wa Mtwara ili kuzungumza na wananchi akiwa anatokea kukagua visima vya
kuzalisha na mitambo ya kuchakata Gesi ya Mnazi Bay iliyopo katika Kata ya
Msimbati wilayani humo.
Wananchi wa Kata ya Msimbati walimweleza
Dkt.Biteko kuhusu changamoto walizonazo ikiwemo barabara, kituo cha afya,
kutopata fedha zozote kutokana na kazi za uzalishaji wa uchakataji Gesi Asilia
unaofanyika kwenye kijiji hicho na kutopata taarifa mbalimbali za mradi ikiwemo
zinapotokea changamoto kwenye bomba la Gesi Asilia.
“Changamoto kwenye miradi hii zinatokea lakini
lazima awepo mtu ambaye ni daraja kati ya Serikali na Wananchi, na Mtu huyu
analipwa mshahara kwa kazi hiyo, haiwezekani Waziri au Rais kuja kutoa taarifa
kwa wananchi wakati kuna mtu kaajiriwa kwa kazi husika, wananchi hawa wanapaswa
kupata taarifa.” Amesisitiza Dkt.Biteko
Katika hatua nyingine, ameagiza Mkurugenzi wa
Huduma kwa Wateja katika Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuondolewa katika
nafasi hiyo kutokana na majibu yasiyo stahiki wanayojibiwa wananchi wanapopiga
simu kwenye Shirika hilo kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali.
Vilevile, Dkt. Biteko ameagiza kuwa, miradi
inapotekelezwa katika eneo lazima ibadilishe maisha ya wananchi, ikiwemo pia
upatikanaji wa huduma za kijamii kama vile Shule, Vituo vya Afya, Barabara na
Maji.
"Changamoto zote mlizozieleza hapa nataka
niwahakikishie kuwa zitashughulikiwa, nataka muone tofauti kuanzia sasa, kama
Gesi Asilia inatoka hapa na inaendesha mitambo ya umeme kwa asilimia 65,
haiwezekani wala haiingii akilini, watu hawa wakalia kituo cha Afya, Polisi,
ubovu wa barabara, haiwezekani, nataka niwaeleze kwamba ushuru wa huduma
unaokusanywa na halmashauri sehemu ya fedha lazima irudi hapa." Amesema
Dkt. Biteko.
Dkt. Biteko, amewaagiza Mkuu wa Mkoa wa Mtwara
pamoja Mkuu wa Wilaya kukaa pamoja na wananchi wa eneo hilo ili mpango wa
maendeleo wa kijiji hicho uandaliwe, hivyo fedha zinapotolewa zifanye maendeleo
kulingana na mpango wa kijiji.
Aidha, ameiagiza TPDC kuweka mpango maalum wa
Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kwa Jamii (CSR) katika eneo hilo ili
wananchi hao waone faida ya kuwepo kwa miradi kwenye maeneo yao na kuwaelekeza
kuwaagiza wajenge kituo cha afya, taa za barabarani na Kituo cha Polisi.
Ili kuhakikisha kuwa, Jamii zinazozunguka na
miradi ya Mafuta na Gesi Asilia zinafaidika na uwepo wa miradi hiyo,
Dkt.Doto.Biteko amesema kuwa Serikali itakuja na kanuni zitakazoongoza masuala
ya CSR lengo likiwa ni kuhakikisha jamii zinazozunguka miradi ya Mafuta na Gesi
zinanufaika.
.jpg)

Post a Comment