Mawaziri wa Afrika
wanaohusika na Masuala ya Fedha na Jinsia kutoka nchi 22 Afrika
wanataraji kukutana nchini Tanzania katika mkutano wa kujadili namna bora ya
kushughulikia athari za mapungufu ya kijinsia katika uchumi.
Nchi zinazotarajiwa kushiriki Mkutano huo utakaoanza Nov,15-17 mwaka huu jijini Dar es salaam ni mwenyeji Tanzania, Burundi, Burkina Faso, Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo, Eritrea, Ethiopia, Guinea, Ivory coast, Nigeria, Senegal, Kenya, Liberia, Madagascar, Malawi, Msumbiji, Somalia, Afrika Kusini, Rwanda, Sudan ya Kusini, Zambia, Zimbabwe na Uganda.
Wakizungumza leo
Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na Waziri wa
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum,Dkt. Doroth Gwajima, wamesema
kuwa mkutano huo unalenga kujadili kuhusu namna yakuwawezesha wanawake na
wasichana kiuchumi na kijamii kupitia ufadhili wa usawa wa kijinsia.
Waziri wa Fedha Dkt
Nchemba amesema mkutano wa Mawaziri utaangazia hatua iliyofikiwa kwenye
utekelezaji wa ahadi zilizowekwa na Jukwaa la Usawa wa Kijinsia, athari za
uchumi jumla katika usawa wa kijinsia na jukumu la upangaji bajeti unaozingatia
jinsia.
‘matokeo yanayotegemewa kwenye mkutano huo wa ngazi ya juu wa Mawaziri ni uwepo wa vipaumbele vya kuharakisha usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake na ahadi ya kugharamia utekelezaji kutoka kwa washiriki wa Mkutano huo’amesema Dkt Nchemba
Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wanawake na Makundi Maalum,Dkt. Doroth Gwajima matokeo
yanayotegemewa kwenye mkutano huo wa ngazi ya juu wa Mawaziri ni uwepo wa
vipaumbele vya kuharakisha usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake na ahadi ya
kugharamia utekelezaji kutoka kwa washiriki wa Mkutano huo.
Mkurugenzi wa IMF Afritac East,Xiangming LI amesema mchango wa wanawake katika uchumi umekuwa mdogo ikilinganishwa na wanaume Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalojihusisha na masuala ya Usawa wa Kijinsia (UN-Women),Hodan Addou akisema Shirika hilo litaongeza ufadhili katika masuala ya usawa wa kijinsia ili kuwawezesha wanawake na wasichana kutoka nchi wanachama
Hata hivyo imeelezwa kuwa matokeo yanayotegemewa kwenye mkutano huo wa ngazi ya juu wa Mawaziri pia ni uwepo wa vipaumbele vya kuharakisha usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake na ahadi ya kugharamia utekelezaji kutoka kwa washiriki wa Mkutano huo.
Post a Comment