PURA: UZALISHAJI WA GESI ASILIA YAFIKIA FUTI ZA UJAZO BILIONI 53.19, 2023

....,...........

Timothy Marko

MAMLAKA ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imesema katika kipindi cha Serikali cha Awamu yasita inayoongozwa na Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan taasisi hiyo imeweza kuimarisha shughuliza kaguzi za katika Mikataba ya Uzalishaji,Ambapo Shilingi bilioni 189 zimeweza kuokolewa na kurudishwa kwenye mfuko wa Serikali nakupelekwa vitalu husika.

Akizungumza katika Mkutano uliowajumisha Waandishi wa Habari na Wahariri jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Mamlaka hiyoMhandisi Charles Sambweni amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imewezesha Ushiriki wa Wazawakatika miradi ya utafutaji na Uzalizaji waMafuta nagesi Asilia nchini.

"Wastani Ushiriki wa Wazawa katika Shughuli za Mkondo wa juu waPetroli kupitia Ajira ni Asilimia 85".Alisema Mhandisi Charles Sambweni.

Mkurugenzi wa PURA Mhandisi Sambweni amesema kuwa taasisi hiyo imeweza kuishauri Serikali kuongeza Muda wa leseni ya utafutaji wa Petroli katika Vitalu vya Tanga,Ruvu,Mtwara Vilivyopo Baharini.

Alisema Taasisi hiyo imeweza kuishauri Serikali na kufanikiwa katika Zoezi la utiliaji Saini kwa mkataba wa Nyongeza wa uzalishaji na Ugawanaji wa mapato ya gesi iligunduliwa katika kitalu cha Ruvuma.

"Mkataba huu utawezesha kuendeleza gesi Asilia kitalu hicho takriban Futi za ujazo Trilioni 1.6Uliosaniwa bainaya wizara ya Nishati TPDC na Kampuni ya ARA ya nchini Omani"Aliongeza Mkurugenzi wa Pura Mhandisi Charles Sambweni.

Mhandisi Sambweni alisisitiza kuwa katika kufanikisha Mikataba wa Ugawanaji wa Mapato kwa lengo la kuhusisha ili kuendana na Mazingira ya uwekezaji katika sekta ndogo ya Mafuta na gesi Asilia.

"Uzalishaji wa gesi Asilia kufikia Futi za UjazoBilioni 53.19 kwa kipindi cha Mwezi julai 2022 hadi February2023 ukilinganisha na futi za ujazo Bilioni 46.96 kwa kipindi kama hicho kwa mwaka 2021/22 Sawa na Ongezeko la Asilimia 14"Alisisitiza Mhandis Charles Samweni.

0/Post a Comment/Comments