SERIKALI KUFANYIA MAREKEBISHO YA SHERIA YA RUSHWA YA NGONO.

........................

 Timothy Marko

SERIKALI imesema inaendelea kufanyia mapitio ya sheria na sera ya vyombo vyahabari huku ikitaka Chama cha waandishi wa Habari wana wawake(TAMWA) kuwa nasubira wakati wanapotafuta ufumbuzi wa changamoto Rushwa ya ngono na ukatili wa kijinsia unalolikumba tasnia hiyo kwa waandishi wa 

Amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ameilekeza wizara hiyo kufanya mapitio ya sera kwa lengo la kuhakikisha tasnia ya habari inafanya vizuri zaidi.

Naibu Waziri huyo aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya miaka 36 ya Chama cha waandishi wa habari Wanawake Tanzania(TAMWA),ambapo pamoja na mambo mengine amesema chama hicho kina mchango mkubwa kwa taifa, ikiwemo kupinga ukatili, kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika ngazi za maamuzi na usawa wa kijinsia.

“Rais Samia ametuelekeza kama wizara kufanyia kazi sera na sheria zilizopitwa na wakati, kama ambavyo tumefanyia marekebisho media service act (sheria ya huduma za vyombo vya habari), niwahakikishie kwamba, katika sheria ambazo zinaenda kutungwa mpya,mawazo yenu na maoni yenu (TAMWA) tumechukua serikali itayafanyia kazi

“Tasnia ya habari imekuwa na changamoto nyingi na Wizara inaendelea kushughulikia kama mabadiliko ya sheria ili kuweza kukidhi upatikanaji wa habari,”alisema

Vilevile Naibu Waziri huyo alisema, serikali inaendelea kuhakikisha kuna uhuru wa kujieleza na wa vyombo vya habari, ndio maana tangu Rais Dk.Samia aingie madarakani hakuna chombo wala mwandishi wa habari aliyefungiwa.

Hatahivyo alisema, katika kuhakikisha wanatasnia ya habari wanafanya kazi kwa weredi, wizara imeundaa kutathimini uchumi wa vyombo vya habari.

Pia Mathew alitoa rai kwa waandishi wa habari wanawake wote nchini kujiunga katika chama hicho, kwa lengo la kukijenga na kuongeza nguvu zaidi.

Vilevile Mhandisi Mathew alikipongeza TAMWA kwa kuwajengea uwezo wanawake katika mambo mbalimbali, ikiwemo kupinga mila na desturi kandamizi

Naye Mkurugenzi wa TAMWA Dk. Rose Reuben,alisema utafiti wao waliyofanya ndani ya vyumba vya habari 22, walibaini wahusika wengi wa unyanyasaji wa kijinsia ni watu wenye mamlaka ndani ya vyombo vya habari wakiwemo wahariri.

Pia Dk.Rose alisema katika kuhakisha wanakabiliana na ukatili ndani ya vyombo vya habari, TAMWA inashirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF),Baraza la Habari Tanzania (MCT) .

Naye Mwenyekiti wa TAMWA Joyce Shebe, alisema wataendelea kutafuta fursa za ndani na nje ya nchi ili kujiinua zaidi na kufanya kazi kwa ukaribu zaidi na asasi za kijinsia.

Alisema TAMWA kwa kushirikiana na asasi nyingine wamepata mafanikio mbalimbali ikiwemo kupitwa kwa sheria ya makosa ya kujamiiana na kuanzishwa kwa sera ya jinsia katika vyombo vya habari, kuongezeka kwa nafasi za wanawke katika vyombo vya habari. 

Aidha pamoja na mambo mengine katika mkutano huo TAMWA ilizindua ripoti ya rushwa ya ngono na ukatili wa kijinsia katika vyombo vya habari nchini.
 

0/Post a Comment/Comments