SHILINGI Trion6.7 Kugharimia Tiba za Magonjwa yasiyo Ambukiza.

....................

Timothy Marko.

KATIKA kuhakikisha sekta ya Afya inamarika ilikuondokana natatizo la Magonjwa yasiyo ambukiza,serikali imetenga shilingi  trioni 6.7katika kuboresha Miundombinu sambamba vifaa tiba ilikukabiliana na Magonjwa hayo.

Akizungumza katika mkutano wa kujadili afua mbalimbali juu yakukabiliana na Magonjwa yasiyo ambukiza jijini Dar es salaam Mkurugezi wa Tiba wizara ya Afya Pascal Lugajohudima amesema kuwa katika kutekeleza Sera ya Afya ya mwaka 2007 Serikali imelenga kushirikiana na watalamu mbalimbali wa nje ya nchi na ndani ya nchi  ikiwemo Asasi za kirahia ilikuweza kupambana na Magonjwa hayo.

"Mwanzoni Mwa Mwezi October Mwaka huu waziri wa Afya Ummy Mwalimu alizindua mpango maalum wa Afya ya Msingi"Alisema Mkurugezi wa huduma za ProfesaTiba Pascal Lugajohudima.

Profesa Lugajohudima amesema moja ya visababishi vya Magonjwa yasiyo ambukiza  ukosefu wa Elimu nakusisitiza kuwa nyenzo muhimu katika kutokomeza ugonjwa huo niutoaji wa Elimu sahihi juu ya Magonjwa ya siyo 

Profesa Lugajohudima alisema kuwa Magonjwa yasiyo ambukiza yanayotokana mtindo wa maisha yamekuwa yakiathiri sana hali za uchumi.

Alisema Lengo lakongamano hilo jijini Dar es salam nikutafutaSuluhisho nakuweka mikakati mbalimbali yakupambana na Magonjwa yasiyo ambukiza.

"Asilimia 67 ya Vifo nchini vinatokana kuwepo kwa magonjwa yasiyo ambukiza na Magonjwa haya yana gharama kubwa katika kupata tiba"Aliongeza Profesa Pascal Lugahudima.

Alisisitiza kuwa Magonjwa kama Shinikizo la Damu huchangia vifo na Magonjwa ya siyo ambukiza nchini.

Naye Mkurugenzi wa taasisi ya MDH Dk David Sando  amesema  katika kuhakikisha taasisi hiyo inapambana na magonjwa yasiyo ambukiza wanaompango wa kutoa huduma za Afya kwa Magonjwa ya siyo ambukiza kwa kuhakisha serikali inatoa Bima ya Afya kwa magonywa hayo sambamba na VVU.


0/Post a Comment/Comments