Dk.HUSSEN MWINYI :USHIRIKI WANAWAKE TAASISI ZA KIFEDHA UMESHUKA.

......................

Timothy Marko .

RAIS wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk.Hussen Ali Mwinyi amesema Hali ya Ushiriki wa Wanawake katika taasisi za kifedha imeshuka kutoka Asilimia 10 kwa mwaka 2017 hadi kufikia Asilimia 4 Mwaka huu.

Akifungua Mkutano wa Hali ya Usawa wa kijinsia   kiuchumi Barani Afrika ukijumuisha Mawaziri wa Maendeleo ya jamii jinsia na Makundi Maalum Pamoja na Mawaziri wa Fedha na Mipango barani Afrika  jijini Dar es salaam Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk Husseni Mwinyi amesema katika kuhakikisha Uchumi wa Bara Afrika unastawi Mwanamke hapaswi kuachwa nyuma.

"Nivyema Sera za Upatikanaji wa Mikopo barani Afrika zifanyiwe Marekebisho ilikuweza kumuinua mwanamke kiuchumi".Alisema Rais Dk Hussen Mwinyi.

Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk Hussen Mwinyi Alisema Ili kuweza kuyafikia Malengo ya Milenia 2063 suala usawa wa kijinsia nivyema Bara la Afrika wakalizingatia.

"SERIKALI ya Awamu ya Sita imeweka Mpango Mkakati kuhakikisha ifikapo 2063 suala laUsawa wakijinsia linazingatiwa katika Nyanja zote  za Maendeleo"Aliongeza DK.Hussen Mwinyi.

Naye Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Wanawake ,jinsia na Makundi Maalum Dorothy Gwajima  amesema  Serikali imedhamiria Usawa wa kijinsia katika nyanja zote.

Alisema Serikali ya Awamu ya sita inatambua nafasi za maamuzi katika kuwawezesha wanawake.

"Haki na usawa wakiuchumi kwa wanawakeni mambo yanayoenda sambamba,Mambo haya lazima yaanzie katika ngazi ya Familia".Alisema Waziri Maendeo ya jamii jinsia na Makundi Maalum Dk.Dorothy Gwajima.

0/Post a Comment/Comments