Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha, na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu
El-maamry Mwamba (kulia) na Balozi wa Sweden nchini, Mhe. Charlotta Ozaki
Marcias, wakisaini Hati za Mkataba wa Msaada wenye thamani ya dola za
Marekani milioni 84 sawa na takriban shilingi bilioni 210, uliotolewa na
Taasisi ya Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE) kupitia Shirika la Kimataifa la
Ushirikiano wa Kimaendeleo la Sweden (SIDA), kwa ajili ya utekelezaji wa
Programu ya Kuimarisha Kada ya Ualimu nchini Tanzania, kuboresha mazingira ya
kujifunza ya wanafunzi kwa kufanya mageuzi katika kada ya ualimu kwa kuzingatia
upangaji na usimamizi wa walimu, kuhakikisha usawa wa kijinsia na
ushirikishwaji, wakishuhudiwa na Afisa Programu wa GPE, Bi. Theresia Moyo na
Mwanasheria kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Leonard Wamala. Hafla hiyo imefanyika
katika ukumbi wa Benki Kuu, jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha, na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu
El-maamry Mwamba (kulia) na Balozi wa Sweden nchini, Mhe. Charlotta Ozaki
Marcias, wakibadilishana Hati za Mkataba wa Msaada wenye thamani ya dola
za Marekani milioni 84 sawa na takriban shilingi bilioni 210, uliotolewa na
Taasisi ya Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE) kupitia Shirika la Kimataifa la
Ushirikiano wa Kimaendeleo la Sweden (SIDA), kwa ajili ya utekelezaji wa
Programu ya Kuimarisha Kada ya Ualimu nchini Tanzania, kuboresha mazingira ya
kujifunza ya wanafunzi kwa kufanya mageuzi katika kada ya ualimu kwa kuzingatia
upangaji na usimamizi wa walimu, kuhakikisha usawa wa kijinsia na ushirikishwaji,
wakishuhudiwa na Afisa Programu wa GPE, Bi. Theresia Moyo na Mwanasheria kutoka
Wizara ya Fedha, Bw. Leonard Wamala. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa
Benki Kuu, jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha, na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu
El-maamry Mwamba (kulia) na Balozi wa Sweden nchini, Mhe. Charlotta Ozaki
Marcias (kushoto), wakionesha hati za Mkataba wa Msaada wenye thamani ya dola
za Marekani milioni 84 sawa na takriban shilingi bilioni 210, uliotolewa na Taasisi
ya Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE) kupitia Shirika la Kimataifa la
Ushirikiano wa Kimaendeleo la Sweden (SIDA), kwa ajili ya utekelezaji wa
Programu ya Kuimarisha Kada ya Ualimu nchini Tanzania, kuboresha mazingira ya
kujifunza ya wanafunzi kwa kufanya mageuzi katika kada ya ualimu kwa kuzingatia
upangaji na usimamizi wa walimu, kuhakikisha usawa wa kijinsia na
ushirikishwaji, wakishuhudiwa na Afisa Programu wa GPE, Bi. Theresia Moyo na
Mwanasheria kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Leonard Wamala. Hafla hiyo imefanyika
katika ukumbi wa Benki Kuu, jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha, na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu
El-maamry Mwamba, akizungumza wakati wa halfa ya utiaji Saini wa Mkataba wa
Msaada wenye thamani ya dola za Marekani milioni 84 sawa na takriban shilingi
bilioni 210, uliotolewa na Taasisi ya Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE)
kupitia Shirika la Kimataifa la Ushirikiano wa Kimaendeleo la Sweden (SIDA),
kwa ajili ya utekelezaji wa Programu ya Kuimarisha Kada ya Ualimu nchini
Tanzania, kuboresha mazingira ya kujifunza ya wanafunzi kwa kufanya mageuzi
katika kada ya ualimu kwa kuzingatia upangaji na usimamizi wa walimu,
kuhakikisha usawa wa kijinsia na ushirikishwaji. Hafla hiyo imefanyika katika
ukumbi wa Benki Kuu, jijini Dar es Salaam.
Balozi wa
Sweden nchini, Mhe. Charlotta Ozaki Marcias, akizungumza wakati wa halfa ya
utiaji Saini wa Mkataba wa Msaada wenye thamani ya dola za Marekani milioni 84
sawa na takriban shilingi bilioni 210, uliotolewa na Taasisi ya Ushirikiano wa
Elimu Duniani (GPE) kupitia Shirika la Kimataifa la Ushirikiano wa Kimaendeleo
la Sweden (SIDA), kwa ajili ya utekelezaji wa Programu ya Kuimarisha Kada ya
Ualimu nchini Tanzania, kuboresha mazingira ya kujifunza ya wanafunzi kwa
kufanya mageuzi katika kada ya ualimu kwa kuzingatia upangaji na usimamizi wa
walimu, kuhakikisha usawa wa kijinsia na ushirikishwaji. Hafla hiyo imefanyika
katika ukumbi wa Benki Kuu, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi ya Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE), Bi. Laura Frigenti,
akizungumza wakati wa halfa ya utiaji Saini wa Mkataba wa Msaada wenye thamani
ya dola za Marekani milioni 84 sawa na takriban shilingi bilioni 210,
uliotolewa na Taasisi hiyo kupitia Shirika la Kimataifa la Ushirikiano wa
Kimaendeleo la Sweden (SIDA), kwa ajili ya utekelezaji wa Programu ya
Kuimarisha Kada ya Ualimu nchini Tanzania, kuboresha mazingira ya kujifunza ya
wanafunzi kwa kufanya mageuzi katika kada ya ualimu kwa kuzingatia upangaji na
usimamizi wa walimu, kuhakikisha usawa wa kijinsia na ushirikishwaji. Hafla
hiyo imefanyika katika ukumbi wa Benki Kuu, jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha, ambaye pia ni Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt.
Natu El-maamry Mwamba (katikati walioketi) na Balozi wa Sweden nchini, Mhe.
Charlotta Ozaki Marcias (wa nne kushoto walioketi), wakiwa katika picha ya
pamoja na ujumbe kutoka ubalozi wa Sweden na Wadau wa Maendeleo, baada ya hafla
ya utiaji saini Mkataba wa Msaada wenye thamani ya dola za Marekani milioni 84
sawa na takriban shilingi bilioni 210, uliotolewa na Taasisi ya Ushirikiano wa
Elimu Duniani (GPE) kupitia Shirika la Kimataifa la Ushirikiano wa Kimaendeleo
la Sweden (SIDA), kwa ajili ya utekelezaji wa Programu ya Kuimarisha Kada ya
Ualimu nchini Tanzania, kuboresha mazingira ya kujifunza ya wanafunzi kwa
kufanya mageuzi katika kada ya ualimu kwa kuzingatia upangaji na usimamizi wa
walimu, kuhakikisha usawa wa kijinsia na ushirikishwaji, iliofanyika katika
ukumbi wa Benki Kuu, jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni, Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi ya Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE), Bi. Laura Frigenti (wa
tatu kushoto walioketi), Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Mhe. Dkt.
Festo Dugange (Mb) (watatu kulia), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na
Teknolojia, Prof. James Mdoe (wa pili kulia walioketi) na Naibu Waziri Elimu,
Mhe. Omary Kipanga (Mb) (wa nne walioketi) na kulia ni Dkt. Emmanuel
Shindika, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Elimu (TAMISEMI). (Picha na
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar es Salaam)
.......................
Na Benny Mwaipaja, Dar es Salaam
Tanzania na Sweden, kupitia Taasisi ya Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE) na Shirika la Kimataifa la Ushirikiano wa Kimaendeleo la Sweden (SIDA), zimesaini Mkataba wa Msaada wenye thamani ya dola za Marekani milioni 84 sawa na takriban shilingi bilioni 210, kwa ajili ya kuimarisha utekelezaji wa Programu ya Kuimarisha Kada ya Ualimu nchini.
Mkataba huo umetiwa saini Jijini Dar es Salaam kati ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha ambaye pia ni Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, na Balozi wa Sweden nchini, Mhe. Charlotta Ozaki Marcias.
Dkt. Mwamba, alifafanua kuwa katika fedha za msaada huo, dola za Marekani milioni 29.3 zitatumika kuboresha mchakato wa ukusanyaji data za elimu; kuboresha elimu ya walimu, ajira, maendeleo endelevu ya kitaaluma, motisha, na uwajibikaji.
Aidha, alisema kuwa dola za Marekani milioni 54.8 zitatumika kufadhili shughuli zinazotegemea matokeo, zikiwa na lengo la kuinua nguvu kazi ya walimu, usawa wa kijinsia, ushirikishwaji, na mazingira ya ufundishaji na kujifunza shuleni ili kuchochea mabadiliko ya kimageuzi kwa kada ya ualimu ambapo itaongeza ufanisi katika mfumo wa elimu ya msingi.
Dkt. Mwamba alisema kuwa Mkataba huo utaongeza jumla ya misaada kutoka GPE nchini Tanzania kufikia dola za Marekani milioni 309, sawa na takriban shilingi bilioni 773 na kwamba fedha hizo zimekuwa nguvu inayoendesha mabadiliko chanya katika mfumo wa elimu, ukigusa maisha ya wengi.
“Tunashukuru kwa michango ya kipindi kilichopita, ambapo Tanzania ilipata misaada kupitia fedha za GPE jumla ya dola za Marekani milioni 225 sawa na takriban shilingi bilioni 562 zilizotumika kugharamia utekelezaji wa programu ya kuimarisha stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu kwa awamu ya kwanza kuanzia 2013 - 2018 na awamu ya pili kuanzia 2019 – 2024” Alisema Dkt. Mwamba
Dkt. Mwamba aliihakikishia Sweden, dhamira ya Serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuendelea kufanya kazi kwa karibu na nchi hiyo, GPE na Washirika wote wa Maendeleo ili kuimarisha ushirikiano wa kimaendeleo.
Kwa upande
wake, Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Charlotta Ozaki Marcias, alisema
kuwa tangu Tanzania ijiunge na Taasisi ya Ushirikiano wa Elimu Duniani (Global
Partneship for Education-GPE), mwaka 2013, sekta ya elimu imeboreshwa ikiwemo
kupungua kwa msongamano wa wanafunzi wa shule za msingi madarasani kutoka wastani
wa wanafunzi 113 hadi kufikia wanafunzi 50.
Alisema
kuwa Serikali yake itaendelea kutimiza wajibu wake wa kuwa wakala wa kutafuta
fedha kwa ajili ya kuiwezesha Serikali kutimiza wajibu wake wa kuboresha mifumo
ya elimu nchini ili kuyanufaisha makundi ya walimu kwa kuwajengea ujuzi,
maarifa, kuwapa motisha, ili kuleta matokeo chanya katika sekta ya elimu.
Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa GPE, Bi. Laura Fringent, aliipongeza Tanzania kwa hatua kubwa iliyopiga katika maendeleo ya sekta ya elimu na kuahidi kuwa Taasisi yake, itaendelea kutoa mchango wa kuboresha mazingira ya walimu nchini ili kuboresha zaidi elimu kwa faida ya maendeleo ya Taifa.
Awali, akitoa maelezo ya mpango huo wa kuboresha elimu kupitia walimu unaofadhiliwa na Taasisi hiyo ya Global Partnership for Education, Naibu Katibu Mkuu-TAMISEMI, Profesa James Mdoe, alieleza kuwa msaada huo utaimarisha zaidi nguvu kazi ya walimu katika kipindi cha miaka minne ijayo kuanzia mwaka 2023/2024 hadi 2026/2027.
Post a Comment