TRA, TANAPA YAIPIGA 'JEKI' TEA


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), CPA, Dk Erasmus Kipesha  Akizungumza katika kikao kazi baina ya wahariri wa mamlaka hiyo. 






                               ********

 Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA),
mesema kuanzia mwaka 2019/20 hadi 2023/24 jumla ya michango na ufadhili wa Sh1.4 bilioni zimepatikana kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa, kutoka kwa wadau mbalimbali.

Wadau hao ni kama vile Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya hifadhi za Taifa (TANAPA) Taasisi ya Asilia Giving inayojihusisha na shughuli za utalii Jijini Arusha pamoja na Taasisi ya Flaviana Matata

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa TEA, Dk Erasmus Kipesha wakati akizungumza na waandishi pamoja na wahariri wa vyombo vya Habari katika mkutano ulioandaliwa na Msajili wa Hazina Jana Jijini Dar es Salaam,

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa  Utafutaji Raslimali na Usimamizi wa Miradi kutoka TEA, Masozi Nyirenda, 
ametaja miradi ya elimu  ambayo imetekelezwa kwa mwaka 2022/23 hadi 2023/24 na kuongeza kuwa Mfuko huo wa Elimu hupokea michango ya rasilimali fedha na vifaa ambapo michango ya fedha hupokelewa kupitia mfumo wa malipo wa serikali (GePG) au kwa njia zingine za kibenki ambazo ni rahisi na nafuu kwa mchangiaji.




0/Post a Comment/Comments