WCF YATOA SOMO AFRIKA

 

                            *******

Mfuko wa fidia kwa wafanyakazi WCF umeendelea kuwa kinara na kuwezesha kuwafanya majirani kutoka nchi za Zambia, Kenya, Botswana, Afrika Kusini na Zimbabwe kujifunza kutoka kwao.

Pia WCF wameendelea kuwa hai kwa kulipa fidia bila kutetereka lakini pia kupata hati safi Kila mwaka tangu kuanzishwa kwakwe mwaka 2015 .

Hayo yamesemwa leo Novemba 2, 2023 na Mkurugenzi Mkuu kutoka Mfuko wa fidia kwa wafanyakazi WCF - Dkt. John Mduma wakati akizungumza na wahariri pamoja na waandishi wa Habari katika mkutano ilioandaliwa na Msajili wa Hazina ambapo alisema asilimia 90 ya huduma zao zinapatikana kwa njia ya mtandao.

"Ulipaji wa fidia kwa wanufaika umeongezeka kutoka kulipa Bilioni 1.55 mwaka 2017 Hadi kufikia kulipa Bilioni 65. 35 mwaka 2023 , Idadi ya madai ya fidia kwa wanufaika waliyopokelewa WCF ni 18,782 na jumla ya madai 14,087 yameshughulikiwa ambapo madai 12,339 yamelipwa, madai 1440 yamekataliwa na madai 308 yamefungwa"

Aidha Dkt. Mduma amesema wamefanikiwa kuimarika uwezo wa kifedha wa mfuko kwa shilingi Bilioni 697.83 kwa mujibu wa hesabu za mpaka tarehe 30 Septemba 2023.

Pia ameeleza kuwa wamefanikiwa kuboresha huduma kupitia usimikaji mifumo ya TEHAMA, Kuboresha kwa kituo Cha huduma kwa wateja na kuboresha tathmini za Ulemavu kupitia mafunzo kwa madaktari.

Kwa upande wa ukusanyaji michango, Dkt. Mduma alisema waajiri wote wanatakiwa kuchangia katika mfuko ambapo waajili Sekta Binafsi 0.5% na waajiri Sekta ya umma 0.5%

Kuhusu utekelezaji wa WCF, Dkt. Mduma alisema "Tunandelea kutoa elimu ili waajiri wanedelee kujisajili, kuangalia vihatarishi maeneo ya kazi, KUTUNZA takwimu ya tulipotoka na tunapoenda ili kuweka mikakati"

Dkt. Mduma alisema majukumu yao ni kusajili kusajili waliopo katika Sekta ya umma na binafsi Tanzania bara, kukusanya michango kutoka kwa waajiri , kutunza kumbukumbu ya ajali, magonjwa na vifo kutokana na kazi na kueleimisha umma kuhusu mfuko wa fidia kwa wafanyakazi.

"Ongezeko la waajiri waliodahiliwa na WCF limeingezeka kwa asilimia 93 kutoka waajiri 5, 178 mwaka 2015/16 hadi kufikia waajiri 31, 467 Septemba 30/2023 na ukusanyaji wa michango kwa waajiri umeongezeka kutoka Bilioni 146.11 mwaka 2015/16 na kufikia Bilioni 758.78 Septemba 30, 2023"

Alisema hayo yanatoka na juhudi za Serikali ya awamu ya Sita chini ya Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri

ya Muungano wa Tanzania kwa kufanya maboresho mbalimbali ikiwemo Kupunguzwa kwa kiwango cha uchangiaji kwa waajiri wa sekta binafsi kutoka kiwango

cha asilimia moja ya awali hadi kufikia asilimia sifuri nukta tano;

Kupunguzwa kwa riba kwa waajiri waliochelewesha michango kutoka asilimia 10

iliyokuwa ikitozwa kwa mwezi hadi kufikia asilimia 2 ya sasa

Pia alisema Kufitiwa riba ya malimbikizo ya michango kwa waajiri waliochelewa kulipa; na

Kuongezwa kwa kima cha chini cha fidia kutoka utaratibu wa awali ambao haukuwa na

kima cha chini cha fidia kwa mfanyakazi ambaye hakupata ulemavu wa asilimia 100 hadi kufikia shilingi 275,702.83 za sasa.

Akifafanua kuhusu Mafao ya fidia Mkurugenzi wa uendeshaji kutoka WCF, Anselim Peter alisema mafao ya Ulemavu wa muda hulipwa mfanyakazi anapopewa mapumziko Zaidi ya siku tatu au kazi nyepesi ambapo hulipwa asilimia 70 ya mshahara ghafi, Kiwango cha chini ni TZS 275,702.83 na hulipwa kwa miezi 24.

Kwa upande wa mafao ya matibabu alisema huanza kulipwa mara (immediately) ajali inapotokea

ambapo aina zote za matibabu hutolewa bila kujali kiwango cha uchangiaji, Mfumo wote wa matibabu Tanzania bara (Bima na Watoa huduma za afya) – hutoa huduma kwa wateja wa WCF, hakuna ukomo wa gharama za matibabu lakini piakuna kifurushi cha matibabu.

Kuhusu mafao ya anayemhudumia mgonjwa, Anselim alisema hulipwa kwa mfanyakazi asiyeweza kumudu kujihudumia, hulipwa asilimia 40 ya pensheni ya mfanyakazi na msaidizi huteuliwa na mfanyakazi.

0/Post a Comment/Comments