CCM YAWATAKA WANANCHI KUTOA MAONI DIRA MAENDELEO 2025-2050, AWAONYA TANESCO .






                                   **********

Timothy Marko

CHAMA cha Mapinduzi(CCM) kimewataka Wananchi kushiriki katika Maoni ya Dira ya Maendeleo 2025-2050.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo, Katibu Mwenezi wa Chama hicho Paul Makonda amesema nivyema wakashiriki katika kutoa maoni ya Dira Maendeleo ya 2050
.
"Tunaomba Wananchi watoe Maoni juu mwelekeo wa Dira ya Maendeleo iendeleje na kwanamna gani"Alisema Katibu Mwenezi Paul Makonda.

Katibu Mwenezi wa CCM Makonda alisema kuwa kinaendelea utaratatibu wake kumtafuta nafasi ya katibu Mkuu iliyoachwa na Abrahamani kinana ikiwemo kukaa vikao vya ndani ya Chama ili kuweza kujaza nafasi hiyo.
Alisema Uchaguzi wa Serikali za mitaa ndio kipimo pekee cha Uhai wa chama na Matawi.

"Tayari Chama kimeshapeleka Madai na Maoni ya Wa chama cha Walimu (CWT) kwa Waziri wa Elimu Profesa Adolf Mkenda" Aliongeza Paul Makonda.

Makonda aliongeza kuwa nivyema kutoa ushirikiano kwa Viongozi waliopo madarakani na walioachwa kwenye Uongozi kwani Uongozi nimfumo wa kupokezana kijiti.

Aliongeza kuwa kuwepo kwenye Makundi ndani ya chama ni mabadiliko ya kimtazamo wa fikra,Nikweli umeme nitatizo hatuja pata mwarobaini ukatikaji wa umeme.

"Kadri ya idadi ya Watu inavyoongezeka Mahitaji yanaongezeka suala umeme tunataka tupeleke Ujumbe kwa Watendaji watendaji wa Tanesco huku sio kumtendea haki kunasababu zingine ni Uzembe  Chama kinauliza Tanesco mnafaa kumuwakilisha RaisDk Samia Samia Suluhu Hassani,"Alisisitiza Paul Makonda.

0/Post a Comment/Comments