DCEA YAKAMATA KG 3,182 YA DAWA ZA KULEVYA


......................

Timothy Marko

KATIKA kudhbiti tatizo la Dawa za kulevya MAMLAKA ya kudhibiti dawa za Kulevya (DCEA) imekamata jumla ya kilogramu 3,182 kutoka kigamboni ambapo watuhumiwa(7) ambapo kati yao wawili wana Asili ya bara la Asia.5

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Kamishina Jenerali wa Mamlaka hiyo Aretas Lyimo amesema kuwa Operesheni hiyo imefanyika tarehe 5 hadi23 Disemba mwaka huu ambapo kiasi hicho kinajumuisha  kilogramu 2,180.29 Aina ya heroni sambamba dawa ya methamphetamine jijini Dar es salaam.

" Kiasi hiki cha ukamataji wa Dawa za kulevya zenye Uzito wa kilogramu 1001.71 aina ya Heroni zilizokamatwa katika wilaya kigamboni,Ubungo,Kinondoni pamoja na9 Wilayaza  mkoani  Iringa"Alisema Kamishina Jenerali (DCEA) Aretas Lyimo.

Kamishina (DCEA) Aretas Lyimo alisema  Ukamataji wa Dawa hizo za kulevya nchini Umeshikarekodi tangu nchi ya Tanzania ipate uhuru tarehe 9 Disemba 1961.

Aliongeza kuwa ukamataji huo wa dawa za kulevya uliofanyika na taasisi hiyo ya umma dawa hizo zilikutwa  kwenye Vifungashio vya bidhaa za majani chai sambamba na kahawa ambapo wasafishaji wa dawa hizo wakiwa lengo ya kutobainika na Watendaji wa mamlaka hiyo.

"Kiasi hiki endapo kingeingia hapa nchini  kiweza kuathiri watu 76,368,000 kwa siku  ukamataji huu umeokoa nguvu kazi,hivyo natoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na mamlaka kwani mafanikio haya nijuhudiza wananchi katika kutoa taarifa" Aliongeza Kamishina (DCEA) Areta Lyimo.

0/Post a Comment/Comments