Na
Abel Paul, Jeshi la Polisi- Arusha.
Jeshi
la Polisi Mkoa wa Arusha limesema kuwa litawakamata na kuwachukulia hatua kali
za kisheria baadhi ya wamiliki wa vyombo vya moto wanatumia kigezo cha mwisho
wa mwaka kuingiza vyombo vyao ambavyo vinachangamoto za kiufundi na kutumia
kigezo cha mwisho wa mwaka kusafirisha abiria maeneo mbalimbali hapa nchini.
Hayo
yamesemwa mapema leo Disemba 03,2023 na Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani
Mkoa wa Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Zauda Mohamed katika kituo
kikuu cha mabasi yaendayo mikoani na nchi Jirani huku akibanisha kuwa
kumekuwepo na tabia ya baadhi ya wamiliki kutumia kigezo cha wingi wa abiria na
mwisho wa mwaka kuingiza magari mabovu barabarani.
SSP
Zauda ameongeza kuwa Jeshi la Polisi kupitia kikosi cha usalama Barabarani
Mkoani humo hakitowafumbia macho wamiliki watakao bainika kuingiza magari
mabovu barabarani huku akisema kikosi
hicho kitaendelea kufanya ukaguzi wa vyombo vya moto mara kwa mara na kutoa
elimu kwa madereva na abiria wanaotumia vyombo hivyo.
Aidha
amewataka madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kumaliza kabisa
ajali ambazo zimekuwa zikisababisha ulemavu na kuwaacha wananchi wakiwa na
ulemavu wakudumu ambapo amewataka madereva ambao wamekuwa wakiendesha umbali
mfupi kuwatumia madereva wazoefu kuwaendesha kama wanakwenda safari ndefu.
Sambamba
na hilo ametoa wito kwa wazazi wanatumia kipindi hiki cha mwisho wa mwaka
kuwasafirisha watoto wadogo Kwenda kuwasalimia ndugu na jamaa maeneo tofauti
tofauti kuhakikisha watoto hao wanakuwa
na uangalizi wa karibu ili kupunguza vitendo vya kupotea kwa Watoto kipindi
hiki cha mwisho wa mwaka.
Kwa
upande wake Mchungaji Getruda Kyando ambaye anatumia usafiri wa mabasi
yanayokwenda maeneo tofauti tofauti hapa nchini Pamoja na kuwaomba Jeshi hilo
kufanya kaguzi za mara kwa mara amekipongeza kikosi hicho kwa kutoa elimu na
mawasiliano ya moja kwa moja kwa abiria ambayo yatasaidia kutoa taarifa kwa
wakati pindi madereva wanapokiuka sheria
za usalama Barabarani.
Nao
baadhi ya madereva wanaofanya safari zao ndani na nje ya nchi wamesema
kumekuwepo na ongezeko la magari kipindi hiki cha mwisho wa mwaka huku
wakiwataka madereva wenzao wasiofuata sheria za usalama barabarani kuhakikisha
wanafuta sheria hizo ili kupunguza ajali hapa nchini.

.jpeg)

.jpeg)

Post a Comment