OSHA YAFUTA ADA, KERO SEHEMU ZA KAZI

Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda akizungumza na wahariri na waandishi wa habari ikiwa ni mwendelezo wa taasisi zilizopo chini ya Ofisi ya Msajili wa Hazina kukutana na vyombo vya habari.



Wahariri na waandishi wa habari kutoka media mbalimbali wakinfuatilia Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda. 
                          *********

Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA), imetangaza kufuta ada zenye thamani ya zaidi ya Sh35 bilioni ili kuboresa huduma sehemu pa kazi. 

Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda alisema hayo jijini Dar es Salaam jana Alhamisi Desemba 7, 2023 wakati akizungumza na wahariri na waandishi wa habari ikiwa ni mwendelezo wa taasisi zilizopo chini ya Ofisi ya Msajili wa Hazina kukutana na vyombo vya habari.

Kwa mujibu wa Mwenda, ada zilizofutwa ama kupunguzwa na OSHA zimeleta unafuu ambao umechochea ukuaji wa biashara na uwekezaji nchini ikiwamo kuongeza ajira kwa Watanzania.

"Ada zilizofutwa ama kupunguzwa zinakadiriwa kuwa zaidi ya Sh35 bilioni na tayari Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza  zitumike katika kuimarisha mifumo ya kulinda wafanyakazi ili waweze kuzalisha kwa tija.

"OSHA kama Taasisi wezeshi, twulifanya mapitio ya mlolongo wa shughuli zetu na kubaini maeneo yaliyohitaji maboresho katika utoaji wa huduma. Miongoni mwa maeneo yaliyokuwa na uhitaji  ilikuwa ni kupunguza au kuondoa baadhi ya ada za huduma ambazo zisingeathiri usimamizi na utoaji wa huduma za usalama na afya mahali pa kazi nchini,"

Alizitaja ada izo kuwa ni pamoja Ada ya Usajili wa eneo la kazi iliyokuwa ikitozwa kati ya Sh50,000 hadi Sh.1, 800,000. Kuondoa Ada ya fomu ya usajili sehemu za kazi iliyokuwa ikitozwa Sh. 2,000 na kufuta faini zinazohusiana na ukosefu wa vifaa vya kuzimia moto ya Sh500,000;

Nyinine ni  Ada ya Leseni ya Ithibati iliyokuwa inatozwa Sh 200,000 kwa mwaka; Ada ya ushauri wa kitaalamu wa Usalama na Afya ya Sh 450,000, Kufuta ada ya mafunzo ya elimu kwa umma iliyokuwa inatozwa Sh250,000 kwa kila mshiriki pamoja na kupunguza ada ya uchunguzi wa ajali iliyokuwa ikitozwa Sh500,000 mpaka Sh120,000. 

"Tumeondoa pia ada ya Kipimo cha Mzio  iliyokuwa ikitozwa Sh25,000 kwa Mfanyakazi, Kipimo cha Kilele cha Upumuaji, Kupunguza ada ya huduma za ukaguzi wa mifumo ya umeme katika vituo vya mafuta vilivyopo vijijini kutoka Sh650,000 hadi Sh150,000. Kuondoa ada ya ukaguzi wa usimikaji wa pampu za gesi kwa kila kituo ambayo ilikuwa inatozwa Sh20,000 kwa kila pampu."

0/Post a Comment/Comments