Kampuni ya michezo ya kubahatisha, Premier Bet imemtangaza mshindi aliyejishindia Tsh Milioni 122,730,200/- ambaye amebashiri matokeo sahihi ya matokeo ya mechi sita kwenye fixture yetu ya Ngumu Kumeza (Halftime/Full time fixture).
Akizungumza na waandishi wa Habari wakati wakikabidhi fedha hizo kwa mshindi wa mchezo huo wa kubahatisha Nurdin Abdalah, Meneja Masoko wa Premier Bet, Eric Kirita amesema Ushindi huu unathibitisha siyo tu uwezo wa kufurahisha michezo ya kubahatisha lakini pia jinsi Premier Bet inavyoweza kubadilisha maisha.
"Tunayo furaha kubwa kutangaza ushindi Mkubwa na wa kuvutia wa Nurdin Abdalah, mshindi wa TSH 122,730,200/- Tsh kupitia michezo ya kubahatisha na burudani ya Premier Bet. Hii ni habari njema na tunayo furaha kuwa sehemu ya safari hii ya kushangaza na Ndugu Nurdin Abdalah".
Kirita amesema wao kama Premer Bet watampa ushauri wa kifedha mshindi huyo ili aweze kuendeleza biashara yake na kufikia malengo.
"Tunampongeza Bwana Nurdin Abdalah kwa ushindi wake mkubwa na tunamtakia mafanikio zaidi katika siku zijazo. Premier Bet inaendelea kujitahidi kutoa uzoefu wa kipekee wa kubahatisha na burudani, na tutampa ushauri wa matumizi ya fedha zake kutokana na biashara anayoifanya"
Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania, Chiku salehe alimtaka mshindi huyo kutumia fedha hizo katika kufanya maendeleo.
"Leo tupo hapa katika kusimamia ushindi wa Nuridin aliyeshinda Milioni 122 ambapo tumefika hapa ili kuthibitisha kuwa ushindi huo ni wa halali na ni sahihi na pia tunathibitisha kuwa pesa zake atazipata kupitia Account yake"
"Tunamshauri Nurdin atumie pesa yake vizuri katika kufanya maendeleo ili kuendeleza nchi yetu"
Amesema mchezo huo wa kubahatisha unachezwa na watu kuanzia miaka 18 kwenda juu na siyo chini ya miaka 18.
Kwa upande wake mshindi wa mchezo wa kubahatisha, Nurdin Abdalah aliushukuru uongozi wa premier Bet kwa ushindi huo kwani kipindi Cha nyuma alikua akicheza na kushinda kiasi kidogo ambapo kwa sasa amefikia hatua ya kupata ushindi mkubwa wa shilingi milioni 122.
"Baada ya kupata ushindi Premier Bet walinipigia kupitia wakala na hawakuzungusha, hivyo nashukuru kwa kunipa ushindi huu "
Amesema fedha zake atazitumia katika biashara yake ya vifaa vya umeme ambayo amekua akiifanya kila siku.
"Mimi ni mfanyabiashara katika upande wa vifaa avya umeme, hivyo fedha hizi ntaziongezea katika biashara yangu nnayoifanya, kupitia ushindi huu unanipa mimi nguvu hata kwenye biashara zangu na hivyo ntafikia ndoto zangu"
Post a Comment