SERIKALI YA WATAKA MAAFISA USTAWI KUJENGA USTAWI FAMILIA KWA KUSHIRIKIANA WIZARA.


 ...,.........,......

Timothy Marko.

SERIKALI imewataka Maafisa ustawi wajamii kujikikita kuimarisha ustawi wa familia nakushirikiana na Wizara ya Maendeleo ya jamii katika kufanya mikutano itakayo leta ustawi wa jamii.

Hayo yamebainishwa na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa jijini Dar es Salaam katika Matimisho ya kilele cha Miaka 50ya Chuo cha Ustawi wa jamii katika Ukumbi wa kimatafa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) ambapo amesema nivyema katika kata na Vijiji kuwatumia maafisa ustawi ilikuweza kuleta jamii iliyobora.

"Utafiti umeonesha Maeneo ya Madini,katika maeneo ya migodi kuna uhitaji mkubwa wa Maafisa ustawi wa jamii,hivi ķaribuni kumekuwa na Vitendo vya kuvunjika kwa ndoa ambapo maafisa ustawi wanahitajika"Alisema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa ⁷alisema kuwa nivyema Wizara ya Maendeleo ya jamii kukamilisha programu ya ulinzi wa jamii kwa kushirikiana Vyuo vyaustawi wa jamii ikiwemo watoto.

"Nivyema Wizara ya Maendeleo ya jamii iandae programu ya Malezi kwa watoto"Aliongeza Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa.

Aidha, Waziri Mkuu Majaliwa alisisitiza kuwa nivyema Wizara idara mbalimbali ikiwemo Asasi za kirahia kutumia Maafisa Ustawi wenye Weledi.

Naye Waziri wa Maendeleo ya jamii,jinsia Wanawake na Makundi Maalum Dk.Dorothy Gwajima amesema Wakati tukielekea kilele cha maadhimisho ya miaka 50 chuo cha ustawi wa jamii,Serikali inatambua Umuhimu wa Maafisa ustawi wa jamii,ambapo amesema Huduma za ustawi wa jamii zilianza tangu 1946 Enzi za ukoloni.

Alisema Katika kipindi cha mwaka 2023/2024 Serikali imelenga kuongeza Ajira kwa maafisa Ustawi ilikuweza kupunguza tatizo la Mmonyoko wa Maadili.

"Tunakwenda kutoa mapendekezo kwenye taasisi kuwapo na Maafisa ustawi ilikuondokana mmonyong'onyoko wa maadili"Alisema Waziri wa Maendeleo ya jamii Dk.Dorothy Gwajima.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii MwajumaTheofique amesema Kamati hiyo imelenga kuweka mafisa ustawi katika balozi zote za Tanzania na kuwataka ofisi za umma kutenga maeneo malumu ya utoaji Huduma za ustawi.

"Nivyema kukawepo maafisa ustawi balozi zetu ilikuleta ustawi wa jamii katika jamii zetu"Alisema Mwajuma Theofìque.

0/Post a Comment/Comments