Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo ametangaza kufuta mshirika Manne na kuyaunganisha 16 ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi serikalini.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es salaam juu ya amuzi huo, Profesa Kitila Mkumbo, ameyataja mashirika yatakayovunjwa kuwa ni Shirika la Uzalishaji la Jeshi la Polisi (TPSCF), Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC), Bodi ya Pareto na Shirika la Elimu Kibaha.
Amesema mashirika yanayounganishwa ni Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) na Wakala wa Udhamini, Utambuzi na Ufilisi (Rita).
Mengine ni Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) na Mfuko wa Pembejeo za Kilimo huku Bodi ya Chai itaunganishwa na Wakala wa Wakulima wa Chai, Bodi ya Nyama ikiunganishwa na Bodi ya Maziwa.
Aidha amesema Profesa Mkumbo amesema Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), kitaunganishwa na Mamlaka ya Maeneo ya Uchakataji Mauzo ya Nje (EPZA), kadhalika taasisi za utafiti za Chai, Tumbaku na Kahawa zinaunganishwa kuwa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (Tari).

Post a Comment