SERIKALI YAJIPANGA KUVILINDA VIWANDA VYA MAGARI NCHINI,RAIS SAMIA ATAJWA MAGARI YA MAHINDRA.



                                      ********


Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imesema ipo mbioni kuifanyia marekebisho sheria ya uagizaji magari nchini ambayo inaruhusu hadi magari chakavu kuingia nchini ili kuzuiaga magari hayo kusaidia kunusuru viwanda vya utengenezaji magari nchini.

Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji,Profesa Kitila Mkumbo,wakati wa uzinduzi wa Magari ya  MAHINDRA  yaliotengenezwa kwa ubia Baina ya kiwanda G truck na Mahindra ya nchini India

Aidha,Profesa Mkumbo,amesema l kwa sasa hapa nchini kumekuwa na viwanda vinavyotengeneza magari hivyo ni wakati wa kubadilisha sheria ya uigizaji magari.

"Sheria ya sasa inaruhusu mpaka magari chakavu yaingie nchini hivyo sheria tutaibadilishe ili kulinda viwanda hivi vinavyozalisha magari hapa nchini"Amesema Profesa Mkumbo.

Hata hivyo,Profesa Mkumbo amesema ujio wa kampuni ya Mahindra ni matokeo ya ziara ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania aliyoifanya nchini India mwezi Octoba mwaka huu.

"Haya ni matunda ya ziara ya Rais Samia nchini India imepelekea ujio wa kiwanda hiki kikubwa kuja kuwekeza hapa nchini"Ameongeza kusema.

Kwa Upande wake,Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha uwekezaji nchini(TIC),Gilead Teri ,amesema kwa sasa hali ya uwekezaji Tanzania ni nzuri huku akiwataka Watanzania kujitokeza kwenye uwekezaji kwa kushirikiana wa wageni kutoka nje.

"Kama wewe Mtanzania unakiwanja,nyumba,shule,kiwanda na unataka ubia na mwekezaji njoo kwetu sisi tutakutafutia uwekezaji na M bia"Amesema Teri.

Huku naye wa GF group,Iman Karmali,amesema wapo nchini kwa miaka 17 na wameweza kutoa ajira za moja kwa moja kwa Watanzania zaidi ya 250 na kubainisha kuwa GF Group na Mahindra mwakani wataanza kuzarisha magari madogo.

0/Post a Comment/Comments