********
WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Nape Nnauye,amesema serikali ipo katika mapitio ya sera Tehama ili kuendana na hali iyopo baada kubainika sera hiyo kunabaadhi ya maeneo kuonekana haiendani na wakati uliopo.
Waziri Nape ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam Wakati wa kusainiwa mkataba wa makubaliano na Kampuni ya kutoka China ya Huawei na Serikali ya Tanzania kuhusiana na masuala ya Teknolojia kwenye vyuo vikuu pamoja na kutoa tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri kupitia mashindano ya Teknolojia yaliofanyakia kwenye vyuo vikuu nchini.
Aidha,Waziri Nape amesema kwa sasa suala la Akiri bandia alikwepeki na ujio wake umekuja na mambo mengi yenye nia hasi.
"Akiri bandia ndio Dunia inavyokwenda na serikali tumeliona hili ndio maana tumeanza kufanyia mapitio ya sera Tehama ili iendana na sasa ili tuwe na sheria ambayo itadhibiti mambo yote hasi yanayotokana na Akiri Bandia"Amesema Waziri Nape.
Hata Hivyo,Waziri Nape ,amewataka vijana nchini kutokuwa nyuma katika teknoloyojia na kudai Dunia ndipo ilipo.
Waziri Nape,ametumia mkutano huo kuwataka walimu wa Vyuo vikuu nchini kuongeza idadi ya wanafunzi wakike kwenye masuala ya Kiteknolojia.
"Utaona hapa nimewambia hapa wawezeshe watoto wa kike kwenye masuala ya Teknolojia,Takwimu za kidunia zinaonesha ushiriki sio mkubwa,nimewambia hapa wawekeze kwenye kuwawezesha watoto wakike kwenye teknolojia"
Kwa Upande wake Makamu mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOM),Profesa Lughano Jeremy Kusiluka,ameipongeza serikali na kampuni ya Huawei kwa hatua ya kuhamasisha teknolojia ya habari kwenye vyuo vikuu nchini na kusema jitihada zinahitajika katika kuhamasisha vijana katika masuala ya Teknolojia ya habari.
"Tunapoelekea katika mapinduzi ya tano ya viwanda hauwezi ukaacha Teknolojia,hivyo tunawataka vijana kujitokeza katika masuala ya teknolojia ili kuweza kujikwamua kiuchumi''Amesema Profesa Kisuluka.
Katika hatua nyingine,Profesa Kisuluka,amewapongeza wanafunzi wa UDOM walioibuka washindi katika mashindano ya masuala ya Teknolojia yaliyoandaliwa na Kampuni na Huawei.

Post a Comment