STEVE NYERERE AWATAKA WADAU,WANANCHI KUCHANGIA TAULO ZA KIKE KWA WAFUNGWA MAGEREZANI.


.................

Timothy Marko

MWENYEKITI wa Taasisi ya Ongea na Mwanao Steve Nyerere Amewataka watanzania kuwachangia huduma za Mswaki na Pedi  Wanawake walioko Magerezani ili kuleta Ustawi wakundi hilo Maalum.

Akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya Programu ya Mama Amstiri Mwanamke jijini Dar es Salaam Steve Nyerere amesema kuwa taasisi ya ke imelenga kutoa taulo kwa Wanawake 1500 walipo Magerezani sambamba nakutoa  Miswaki kwa kundi hilo Maalumu.

"Tumekuwa tukichangia Harusi na kutoa Zawadi na kufanya Birthday  lakini tumelisahau kundi hili".Alisema Steve Nyerere.

Steve Nyerere alisema kuwa Sio kilamtu aliyeGerezani anahatia, nakutaka jamii kundi hilo kupewa kipaumbele katika kulisaidia kundi hilo.

Alisema Pedi zitakazotolewa hatizotolewa mashuleni tu,bali taasisi hiyo imelenga kutoa Pedi kwa wanawake waliopo katika Magerezani kote nchini.

"Pedi hii ya Mama itamfikia kila Mtu tunalenga kutoa pedi10 kwa kila mtu kwamiezi kumi,Ninachokiomba tusidumbukize Siasa kwenye Afya za Watanzania"Aliongeza Steve Nyerere.

Naye Mwenyekiti  wa Taasisi ya Loves Foundation Lovenes Mamuya amesema taasisi yake inaendelea kumshika mkono katika Masuala ya Wanawake waliopo Magerezani.

Alisema Mwanamke ni kiumbe ambaye ana hitaji hali yausafi katika Mwiliwake ili aonekane nadhifu mbele ya jamii,hivyo utoaji wa taulo za kike kwamwanamke nijambo Muhimu.

'" Ninatoa Wito hasa kwa Waandishi wa Habari najamii nzima muweze kutusapoti katika hili"Alisema Mratibu Loves Mamuya.

0/Post a Comment/Comments