TANDALE SACCOS YAWATAKA WATANZANIA KUCHANGAMKIA FURSA YA MIKOPO,

 

                           

                               *******


WATANZANIA wameshauriwa kujiunga kwenye SACCOS kwa ajili ya kujipatia mikopo ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Rai hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na  Meneja wa Tandale Saccos,FrorenceRose J Mzoo,wakati wa mkutano mkuu wa Saccos hiyo ambao ulikuwa na malengo mbalimbali ikiwemo kupokea taarifa ya mwaka pamoja na uchaguzi wa nafasi mbalimbali.

Aidha,Mzoo,amewataka vijana,wamama,kujitokeza kwa ajili ya kujipatia mikopo kwenye saccos hiyo.

"Mikopo tunayoitoa hapa ni riba nafuu,na tunatoa mikopo mbalimbali hata kwa wakina mama ,wanatakiwa wawe vikundi kwaanzia watatu"Amesema Mzoo.

Hata hivyo,Mzoo .amesema katika kuhakikisha wanawafikia wakazi wa Dar es Salaam,wamefanikiwa kufungua matawi sehemu mbalimbali ikiwemo Tip Top pamoja na Buza. 

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Tandale Saccos,Abdallah Seifu Salum,amesema kwa kipindi cha uongozi wake wameweza kutatua changamoto mbalimbali

0/Post a Comment/Comments