WAKAZI WA MBEZI JUU WAILILIA SERIKALI ADHA KELELE NYAKATI ZA USIKU


 .....................

Na Mwandishi Wetu,

WAKAZI Wa Mbezi juu Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es salaam wameiomba serikali kuingilia kati kelele zilizopitiliza  kwenye Makazi yao kutokana na watoto kushindwa kusoma pamoja na wagonjwa kukosa usingizi

Wakazi hao wa Mbezi juu, mtaa wa Mbezi Wani. Maeneo ya Vodacom data center wamesema kelele zimekuwa nyingi na kuathiri watoto ambao wanajisomea kujiandaa na masomo msimu ujao 2024,  "tunateswa sana na Bar inaitwa 4U EXECUTIVE pamoja na baadhi ya makanisa ambayo yanashindana usiku kucha,  tulishawaita watalaam kutoka Manispaa ya kinondoni lakini wakakaidi wito na kufika Katika ofisi za Mazingira ili hali hawana hata Leseni za biashara" 

Kamazola Ullomi mkazi wa Mbezi anasema wenye mabaa hawana leseni za kuuzia vileo na kusababisha adha kubwa  kwa wananchi, wenye baa wamegeuze eneo ukumbi wa disko la wazi. Hatuna ahuweni, Muziki wao ni kelele jumatatu mpaka Jumapili, Tunashindwa kupumzika, watoto hawasomi. hatulali kwa amani, alisema mkazi huyo

Hivi karibuni mkurugenzi mkuu wa NENC Mhandisi Samuel Gwamaka Mafwega aliwataka wamiliki wa Baa na Kumbi za starehe kuendesha shughuli zao bila kufanya uchafuzi wa kelele kwa wananchi wanaokaa karibu na shughuli hizo, aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini,

Alisema kuwa “Baraza la Taifa na Usimamizi wa Mazingira limekuwa likipokea malalamiko mengikutoka kwa wananchi kuhusu kero na usumbufu mkubwa wanaopata kutokana na kelele kutoka kwa baadhi yenu mnaoendesha shughuli hizo”

Kutokana na kelele hizo zinazolalamikiwa Baraza limejipanga kutoa elimu kwa wadau wote wanaomiliki vyombo hivyo vya starehe ili kuwapa elimu juu ya namna ya kudhibiti kelele hizo ili zisiwe kero kwa wengine. Kulingana na shughuli hizi kufanyika katika makazi ya watu baraza halinabudi kuandaa mikutano mbalimbali nchini kuwaelimsha wamiliki kutumia chombo cha udhibiti wa kelele kuepuka malalamiko yanayotolewa na wakazi wa maeneo husika. Kutokana na hayo, Baraza limeanza kutoa elimu kwa wamiliki wa baa na kumbi za starehe kwa mkoa wa Dar es Salaam na kufuatiwa na Mkoa wa Pwani.

Bugudha inayotokana nakelele, mbali na tafiti na chambuzi mbalimbali imethibitisha kuwa kelele hizo zina athari kubwa kwa wananchi ikiwemokukosa usingizi, wazee na wamama wajawazitokukosa kupumzika vizuri wakati wa mchana na usiku, presha, ukiziwi hata hivyo zinaathari kubwa kwa wanaume zinapelekea kupungua kwa nguvu za kiume.

Aidha, alitoa kifungu cha Sheria ambacho kilitangazwa katika gazeti la serikali (GN) Namba 32 la tarehe 30 January, 2015. Kanuni hizi zilitungwa kwa mujibu wa kifungu namba 230 (2) (s) cha sheria ya Usimamizi wa Mazingiraya Mwaka, 2004

0/Post a Comment/Comments